Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Balozi Mushi (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake wajasiriamali kutoka katika masoko ya jijini Dar es Salaam ambao wapo ndani ya Shirika la EfG ambao wapo katika ziara ya kuwahamasisha wanawake wafanyabiashara masokoni wa mkoa huo kujiunga katika umoja wa kitaifa.
Afisa mradi wa shirika EfG, Susan Sitta akimkabidhi mfuko wenye machapisho mbalimbali kutoka EfG, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Balozi Mushi.
Meya wa Manispaa ya Mkoa wa Mtwara, Geofrey Mwanchisye (kushoto), akiwa amebeba mfuko wenye machapisho mbalimbali kutoka EfG.
Wanawake wajasiriamali kutoka katika masoko ya jijini Dar es Salaam ambao wapo ndani ya Shirika la EfG wakimsikiliza Meya wa Manispaa ya Mkoa wa Mtwara, Geofrey Mwanchisye (hayupo pichani)
Meya wa Manispaa ya Mkoa wa Mtwara, Geofrey Mwanchisye (wa tatu kutoka kulia walioka), akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake wajasiriamali kutoka katika masoko ya jijini Dar es Salaam ambao wapo ndani ya Shirika la EfG ambao wapo katika ziara ya kuwahamasisha wanawake wafanyabiashara masokoni mkoa huo kujiunga katika umoja wa kitaifa.
Na Mwandishi Wetu, Mtwara.
WANAWAKE wajasiriamali katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo (Sauti ya Mwanamke Sokoni) wameiomba halmashauri hiyo kuwaboreshea mazingira ya vyoo kwenye kazi zao hizo hususani matundu ya vyoo kwani yaliyopo ni machache ikilinganishwa na uwingi wao.
Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki na wanawake hao wakati wa ziara ya mafunzo kwa wajasiriamali hao iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na shughuli ya kuinua maendeleo ya sekta isiyo rasmi hapa nchini hasa kwa wanawake la Equality for Growth (EfG ) lenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo yameambatana na kutambulishwa kwa mradi huo wa Sauti ya Mwanamke Sokoni mkoani hapa wenye lengo la kuhamasisha wanawake wafanyabiashara katika manispaa hiyo na mkoa kwa ujumla kujiunga na umoja wa wanawake sokoni wa kitaifa ambapo kwa sasa Mtwara mradi unatekelezwa kwenye Soko Kuu, Saba saba pamoja na Magomeni.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake kutoka Soko Kuu la Mtwara Magdalena Malembe alisema masoko yao kwa sasa yanakabiliwa na changamoto hiyo kutokana hayana vyoo vya kutosha kwani wanawake wametengewa matundu mawili ya vyoo sokoni hapo lakini tundu moja tu ndio linalotumika.
“Halafu humo humo sisi wanawake huwa tunakutana na changamoto kwani wanaume wanaingia mle mle kwenye chumba chetu inatukwanza lakini kwa vile sisi inaonekana ni viumbe dhaifu basi tunatumia hivo hivo”,Alisema Malembe
Hata hivyo ameongezs kuwa, ” Ila halmashauri yetu mnapaswa mtambue sisis akina mama wafanya biashara wa sokoni tunafanya kazi katika mazingira yasiyo rafiki”,
Wanawake hao ni viwanda lakini pia wanazalisha Taifa kwani rasirimali watu hutokana na akina mama kwahiyo shimo hilo moja la choo huingia akina mama hao na watoto sssa wakiingia akina baba huwa wanaharibu mazingira hivyo upo uwezekano mkubwa watu hao kuweza kupata madhara kiafya.
Charles Chambea, Katibu wa Soko la Saba saba ametilia mkazo na kusisitiza juu ya changamoto hiyo na kwamba kutokana na uwingi wa wajasirimali hao kwa siku za usoni halmashauri kuona umuhimu wa jambo hilo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitoka kwa watu hao.
Afisa mradi wa shirika hilo Susan Sitta alisema, mradi huo unalenga kuwakomboa wanawake kwani wanaonekana kupata faida, thamani ndogo ya bidhaa zao na wengi wao wanapata chini ya shingi elfu 7000/- kwa siku na asilimia 86.2 hawabaki na kiasi chochote au hubaki na kiasi kudogo kwa ajili ya chakula na mahitaji ya lazima.
Meya wa Manispaa hiyo Geofrey Mwanchisye amewatoa hofu na kuahidi kufanyiwa kazi changamoto hiyo inayowakabili wajasiriamali katika maeneo hayo huku akiwaomba kuwa na matumaini katika hilo.
Mradi huo kwa sasa unatekelezwa katika mikoa tisa hapa nchini ikiwemo Iringa, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Lushoto-Tanga, Musoma, Lindi, Mtwara na Dar es salaam yenye jumla ya wanachama 6500.