Home Mchanganyiko TMDA YAFANYA UKAGUZI KATIKA VITUO VYA UTOAJI HUDUMA ZA DAWA NA VIFAA...

TMDA YAFANYA UKAGUZI KATIKA VITUO VYA UTOAJI HUDUMA ZA DAWA NA VIFAA TIBA NA KUGUNDUA BAADHI YA DAWA BANDIA

0

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw.Akida Khea akizungumza na Wanahabari leo katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za TMDA Jijini Dar es Salaam.

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) limefanya ukaguzi katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za Afya zikiwemo dawa na kugundua kuwepo kwa dawa bandia na kuzishikilia.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw.Akida Khea amesema kuwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019, baadhi ya dawa bandia zilizobainika na kutolewa taarifa ya kuwepo katika nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na dawa aina ya Gentrisone Cream 10gm toleo namba GNTRO X030,Augmentin 625mg tables toleo namba 786627 na kapsuli za Cold caps.

“Viwanda halisi vinavyotengeneza dawa hizi vilithibitisha kuwa dawa hizo hazikutengenezwa na viwanda huzika. Amesema Bw.Khea.

Aidha, Bw.Khea amesema kuwa kwa mujibu wa uchambuzi na uchunguzi uliofanywa na TMDA, matoleo ya dawa hizo husika yalithibitishwa kuwa ni bandia.

“Uchunguzi kupitia maabara ya TMDA kwa dawa ya Gentrisone cream 10gm toleo namba GNTRO XO30 ulionesha kuwa dawa hiyo haikuwa na viambato hai (active pharmaceutical ingrediets) vya dawa hiyo ambavyo ni Betamethasone Proprionate, Clotrimazole na Gentamycin sulfate”. Ameongeza Bw.Khea.

Hata hivyo Bw.Khea amesema kuwa katika operesheni ya ukaguzi katika Mikoa inayopakana na nchi za jirani ikiwemo mikoa ya Kigoma,Songwe,Kagera,Rukwa, Mbeya,Mara,Kilimanjaro, Arusha,Mwanza, Ruvuma,Mtwara na Tanga. Wakati mikoa mengine ni Dar es Salaam,Dodoma,Shinyanga,Geita,Singida ,Morogoro,Iringa, na Tabora

“Katika operesheni hii jumla ya maeneo 558 ikiwa ni famasi 209,maduka ya Dawa Muhimu 263, Vituo vya kutolea huduma za afya 27,Maduka ya Vifaa Tiba 21 na Vituo vya dawa asili na tiba mbadala 38 katika”. Ameongeza Bw.Khea.

Kwa upande wake Mratibu wa Polisi toka CID HQ, Bi. Alekunda Urio amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kuzifuatilia kesi hizo kwa  karbu kesi zilizofungunguliwa na TMDA na kuhakikisha watuhumiwa wanachukuliwa hatua za kisheria na TMDA kwa wale wote ambao wamekutwa wakimiliki dawa bandia.