Home Mchanganyiko WADAU KANDA YA ZIWA WATOA MAONI SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA...

WADAU KANDA YA ZIWA WATOA MAONI SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA

0

Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi  Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara akifungua kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Grace Mwangwa akitoa maneno ya awali kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Mshauri Elekezi Prof. Linah Mhando akifafanua jambo kwa Wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia katika kikao kilichowakutanisha na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Wadau wa Maendeleo ya Wanawake na Jinsia wakifuatilia majadiliano katika kikao kilichowakutanisha na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Wadau wa Maendeleo ya Wanawake na Jinsia wakifanya majadiliano katika kikao kilichowakutanisha na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

………….

Na Mwandishi Wetu Mwanza

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na wadau wa maendeleo ya wanawake na Jinsia kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kufanya tathimini ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 na Mkakati wa utekelezaji wa mwaka 2005 ili tathimini hiyo isaidie kufanya mapitio na maboresho ya Sera itakayozingatia makubaliano ya mikataba mbalimbali, Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano.

Haya yameelezwa leo mkoani Mwanza na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Grace Mwangwa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau wa maendeleo ya wanawake na Jinsia kutoka mikoa ya Mwanza. Mara, Kagera, Geita, Simiyu, Shinyanga na Kagera na Wizara.

Bi. Grace amesema Wizara ndio yenye jukumu ya utekelzaji wa Msualaya jinsi nchini yanazingatiwa na hivyo ili yaweze kutekelzwa yanahitaji kuwa na Sera na Mikakati ni muhimu katika kuleta maendeleo ya wanawake na jinsia.

Amesisitiza kuwa madhumuni ya Sera iliyopo yalikuwa ni kutoa mwelekeo ambao ungehakikisha kuwa mipango, Mikakati na shughuli mbalimbali za uongozi na maendeleo katika kila Sekta na Taasisi inazingatia usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa lengo kuu la kupitia Sera hiyo ni kuifanya iendane na wakati na iwezi kubeba mabadiliko yaliyojitokeza katika miaka kumi na tisa tangu kuandaliwa kwake mwaka 2000 ikiwemo changamoto katika utekelezaji wa Sera hii ikiwemo mapungufu yake na nini kifanyike ili kuiboresha Sera ili kueandana na wakati husika.

“Tunahitaji kupata maoni yenu tunahitaji maelekezo yenu nini hakikuzingatiwa tunaomba maoni yenu ili tuwe na Sera itakayosaidia maendelo ya Waanwake na Jinsia nchini ”Alisema  Bi. Grace

Bi Grace ameongeza kuwa bali na kukutana na wadau na kupata maoni pia watakutana na vikundi vya kijamii na mwananchi mmoja mmjoja kwa kupita katika baadhi ya vijiji vya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuwafuata walipo ili kuweza kupata maoni yao ili kuweza kiboresha Sera hiyo.

Akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji  Bw. Emil Kasagara amesema kuwa Kikao hicho kinatarajia kufikia malengo ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake katika kufikia maendeleo jumuishi hususan katika Sekta ya Afya, Elimu, Kilimo na Masuala ya kifedha, uwezeshaji wa wanawake katika nafasi za uongozi na siasa, mazingira na Uzazi na Afya ya Mtoto na kukusanya Taarifa na Takwimu zitakazowezesha kuandaa Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia.

Ameongeza kuwa kikao kazi hicho kitawezesha kukusanya maoni yatayowezesha kuwa na Sera Shirikishi inayozingatia masuala yote muhimu na kupata uelewa wa pamoja kuhusu wajibu wa Serikali na wadau  katika uwepo wa Sera ya maendeleo ya Wanawake na Jinsia .

“Natumai mtatumia muda huu vizrui kujadiliana na kupata maoni yatakayowezesha kupata Sera mbayo itakuwa imekidhi mahitaji ya wakati tulionao na hata kuhakisi yatakayojitokeza hapo mbele” Alizema Bw. Kasagara

Mshauri Elekezi Prof. Linah Mhando ameeleza  maeneo yanayopewa kipaumbelekatika Sera mpya ni Jinsia na maendeleo ya Mji/Vijiji, Jinsai na haki za umiliki ardhi, Jinsia, maji na usafi wa mazingira, Haki za mtoto wa kike, Jinsia na ulemavu, Ukatili wa Kijinsia,jinsia, sayansi ,teknolojia na ufumbuzi , Jinsia, afya uzazi na Ukimwi, Jinsia, uongozi na maamuzi, Jinsia, ajira na kazi, Jinsia, Sheraia na haki za binadamu na Jinsia na hifadhi ya jamii.

Ameyataja maeneo mengine kuwa ni Jinsia na kuwawezesha wanawake kiuchumi, Jinsia na ujumuishwaji wa kifedha, Jinsia na mabadiliko ya tabianchi,Jinsia na Nishati, Jinsia na Miundombinu, Jinsia na Takwimu, Jinsia na Madini, Jinsia na vyombo vya habari na Mawasiliano, Jinsia na Mila na Desturi, Jinsia na Jmii za ufugaji, Ufadhili na Jinsia na Jinsia na uvuvi.

 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipo katika machakato wa kukusanya maoni kwa wadau kutoka Kanda saba za Tanzania Bara ili kuwezesha maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Mwaka 2000.