Home Mchanganyiko George Misafi Awataka Vijana Kuwa Msaada Kwa Rais Dkt Magufuli kwa kufanya...

George Misafi Awataka Vijana Kuwa Msaada Kwa Rais Dkt Magufuli kwa kufanya kazi

0
Mkurugenzi  wa kampuni ya mabasi  ya  Misafi ,George Misafi (kushoto) akimkabidhi  mwenyekiti  wa umoja  wa vijana  wa chama cha  mapinduzi (UVCCM)  kata  ya Makorongoni  mjini Iringa  Steven Chaula msaada wa  shilingi 500,000 kwa  ajili ya  kununua vifaa vya  vijana (picha na Francis Godwin)

…………………..
Mkurugenzi   wa kampuni ya  mabasi ya Misafi  George Misafi  amewataka   vijana   nchini  kufanya kazi  zenye  tija kwa  ajili ya  kumsaidia Rais Dkt John Magufuli   kujenga  uchumi wa  Taifa kwa  kutumia raslimali  za  Taifa  badala ya  vijana  kushinda  vijiweni pasipo  kufanya kazi.
Akizungumza  jana  wakati  akiwakabidhi  kiasi cha  shilingi 500,000 za kununua  vifaa vya    umoja  wa vijana   wa  chama  cha mapinduzi (UVCCM)  kata  ya Makorongini  mjini  Iringa  ,Misafi  alisema  kuwa  jukumu  kubwa la  vijana  ni  kufanya kazi zenye  tija  ya  kiuchumi  ili  kusaidia  kulipeleka Taifa  mbele na sio  vijana   kuwa  watu wa  kulalamika  mitaani .
Misafi  ambae  amepata  kuwa  katibu mwenezi wa    chama  cha  mapinduzi (CCM)  kata ya Makorongoni  alisema  kuwa   jitihada  kubwa  zimekuwa zikifanywa na Rais Dkt Magufuli katika  kuwaletea maendelea  watanzani tena kwa  kuwajali  wanyonge   zaidi .
Lakini  wapo  baadhi ya  vijana  ambao  wao  mbali ya  kuwa na fursa  za  kuondokana na hali ya umasikini ama  kati ya  makundi ya  watu  wanaolalamika  hali  bila  kufanya kazi ila  vijana  hao  wamekuwa  mbele   kuongoza makundi ya wanaolalamika jambo mbalo si sahihi .
” Rais wetu  Dkt Magufuli  amekuwa  mbele  sana kulipeleka Taifa  kwenye  uchumi  wa kati  kwa  kujenga miradi  mbali mbali ya  kiuchumi nchini tumeona miradi  ya umeme ,Hospitali  kila  wilaya ,barabara ,maji  ,,ununuzi wa ndege ,mashule na miradi  mbali mbali  mikubwa  ambayo yote  kwa ajili ya  watanzania  ila  vijana  badala ya  kuibua  miradi yetu  wenyewe  tumebaki  kulalamika  mitaani  si  sawa na hatumtendei haki Rais na  serikali  yetu ” alisema
Jukumu   kubwa la  vijana ni  kuungana pamoja na  kufanya kazi  zenye  tija  na  pale  ambapo  unahitajika  msadaa  ama  nguvu  kutoka   serikalini  kuweza  kutumia vikundi  vya  vijana  walioungana  pamoja   kuomba serikali kuongeza  nguvu na sio  kushinda  kulalamika  pasipo  kuwa na  shughuli za  kufanya .
Akitolea  mfano  alisema kwa   upande  wake  ni kijana  kama  vijana  wengine  ambao wamekulia ndani ya chama  na kufanya kazi za chama  ila pamoja na  kukitumikia chama   sasa ameweza  kujiongeza  na  kutafuta mtaji  wake  wa  kununua mabasi zaidi ya  moja na kuamua  kufanya kazi ya usafirishaji .
Misafi  alisema mbali ya  kuwa amehama  mkoa wa  Iringa  na kuhamia mkoani  Dodoma  kwa    shughuli  zake  za kibiashara  ila bado  anaendelea   kuwakumbuka  vijana  wa  mkoa wa Iringa kata   hiyo ya Makorongoni ambao  walitokea kumwamini  na  kumchagua   kuwa katibu  mwenezi  wa CCM  wakati akiwa mgeni  kutoka wilaya ya Imalinyi  mkoani Morogoro  ambako  ndiko alikozaliwa .
Alisema  amelazimika  kuendelea  kuwajali vijana hao  kwa kuwa anatekeleza ilani ya CCM na alipata  kuwaahidi  kuwasaidia  na  anatarajia  kuwatafutia  mradi  wa  kiuchumi  wa  kufanya  utakaowaingizia  pesa  vijana wa Makorongoni .
Kwa  upande wake  katibu  kata wa CCM kata ya Makorongoni  Jonhson  Dick  pamoja na  kupongeza msaada  wa  Misafi  kwa vijana  hao  bado  alisema   vijana  wanaowajibu  wa  kuendelea   kuunga mkono   jitihada za  serikali ya CCM kwa  kuhakikisha  wanashiriki uchaguzi wa  serikali za  mitaa na uchaguzi mkuu  mwaka 2020 kwa  kuchagua  viongozi wanaofanana  na Rais Dkt Magufuli