Home Mchanganyiko KATIBU WA BUNGE NDG. KAGAIGAI AKUTANA NA JAJI MSTAAFU DE MELLO, VIONGOZI...

KATIBU WA BUNGE NDG. KAGAIGAI AKUTANA NA JAJI MSTAAFU DE MELLO, VIONGOZI WA MISA – TAN BUNGENI JIJINI DODOMA

0

Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilihusu ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya katibu wa Bunge na MISA TAN.

Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akizungumza na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (katikati) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilihusu ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya katibu wa Bunge na MISA TAN, ugeni huo ulioongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania, Ndg. Gasirigwa Sengiyumva (wa pili kulia)

Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akisalimiana na Viongozi wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) kabla ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilihusu ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya katibu wa Bunge na MISA TAN.