Home Mchanganyiko JAFO AZITAKA AZAKI KUTANGAZA MAENDELEO YANAYOFANYWA NA SERIKALI KWA WANANCHI

JAFO AZITAKA AZAKI KUTANGAZA MAENDELEO YANAYOFANYWA NA SERIKALI KWA WANANCHI

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji, Wajibu, Bw.Ludovick Utuoh,kabla ya kufunga  Mkutano wa Mijadala ya wiki ya AZAKI iliyohitimishwa leo jijini Dodoma baada ya kuanza Novemba 4 hadi 8 mwaka huu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akizungumza,na wadau kutoka Asasi za Kiraia wakati akifunga Mkutano wa Mijadala ya wiki ya AZAKI iliyohitimishwa leo jijini Dodoma baada ya kuanza Novemba 4 hadi 8 mwaka huu.

Rais wa Foundation for Civil Society, (FCS), Dkt Stigmata Tenga,akitoa taarifa kuhusu jinsi Wiki ya AZAKI ilivyokuwa katika maonesho hayo ambayo yalianza Novemba 4 hadi leo Novemba 8 ambapo yamefungwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM Mhe.Humphrey Polepole,Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa majadiliano ya Wiki ya AZAKI ambayo yalianza jijini Dodoma Novemba 4 hadi leo Novemba 8.

Mkurugenzi Mtendaji, Wajibu, Bw.Ludovick Utuoh, Akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya wiki ya AZAKI ambayo yalianza jijini Dodoma Novemba 4 hadi leo ambapo yamefungwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akisisitiza jambo kwa washiriki kutoka  Taasisi mbalimbali  za Asasi za Kiraia wakati akifunga Mkutano wa Mijadala ya wiki ya AZAKI iliyohitimishwa leo jijini Dodoma baada ya kuanza Novemba 4 hadi 8 mwaka huu.

Sehemu ya washiriki wa Taasisi za Asasi za Kiraia wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati akifunga maonesho ya wiki ya AZAKI yaliyomalizika leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya uwezeshaji Asasi za kiraia(FCS), Francis Kiwanga,akizungumza na washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Asasi za Kiraia wakati wa kufunga mkutano wa majadiliano ya wiki ya AZAKI.

Mratibu ,Wiki ya AZAKI 2019 Justice Rutenge,akitoa taarifa ya hitimisho ya Wiki ya AZAKI ambapo maonesho hayo yamefikia mwisho na kufungwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo yalianza jijini Dodoma Novemba 4 hadi leo Novemba 8,2019.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Asasi za Kiraia (AZAKI) ambapo maonesho hayo yameitimishwa leo jijini Dodoma.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

…………….

Na Alex Sonna.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Seleman Jafo amezitaka Asasi za kiraia(AZAKI) nchini kutangaza maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli ili wananchi waweze kuyafahamu badala ya kuzungumzia mabaya peke yake.

Aidha, ameagiza mikoa na halmashauri kuhakikisha zinatoa vibali vya usajili kwa asasi hizo ili ziende kufanya kazi za kuleta maendeleo nchini.

Jafo ametoa maagizo hayo leo alipokuwa akifunga kongamano la wiki ya AZAKI, jijini Dodoma.

Amesema ni vyema asasi hizo zikatangaza mambo mema yenye ukweli ndani yake badala ya kutangaza mabaya wanayoyasikia bila kujua ukweli uliopo.

“Wapo wachache wanaojaribu kupotosha ukweli nyie msiwaige kwa sababu nyie ni watu wa kuleta chachu ya maendeleo na kutangaza jitihada za maendeleo zinazofanywa na serikali, ” amesema Jafo.

Amesema kuna umuhimu wa AZAKI kueleza mambo mazuri ya maendeleo yanayotekelezwa kwa kuwa yametokana na mchango wao wa kuibua changamoto zilizopo katika sekta mbalimbali hapa nchini.

 “Naomba niwapongeze sana AZAKI mmekuwa mkiibua matatizo yaliyopo sehemu tofauti, kwa mfano Hakielimu na tangazo lao la shule mbovu,yamesaidia serikali imeona na kuwekeza fedha nyingi katika sekta ya elimu kwa ajili ya kuziboresha na kufanya ujenzi,” amesema.

Aidha amesema katika sekta ya afya na barabara kero mbalimbali zimeibuliwa na serikali imezifanyia kazi yote na kuzifanya sekta hizo kuimarika.

Ameziagiza asasi hizo kuhakikisha wanasaidiana katika kuwezeshana na kurekebishana na sio kusemeana vibaya ili asasi nyingine zife jambo ambalo halikubaliki.

Kuhusu utoaji vibali, Jafo amemuagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha anasimamia utoaji wa vibali vya usajili wa asasi hizo.

“Sitaki kuona ama kusikia malalamiko yeyote kuhusiana na kukwama kwa vibali vya usajili ninachotaka kusikia ni asasi zimepewa vibali ili mradi tu vina sera na muongozo inayohitajika ndani ya serikali,”amesisitiza.

Naye, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole , amesema AZAKI na Serikali ni kitu kimoja hivyo haina haja ya kuogopana kama kuna suala lolote la wanapaswa kukutana na kulipatia ufumbuzi.

Kwa upande wake,  Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya uwezeshaji Asasi za kiraia(FCS), Francis Kiwanga, amesema AZAKI ipo kwa ajili ya kujenga na sio kubomoa kama baadhi ya watu wanavyofikiria.