Home Mchanganyiko Mradi Hospitali ya Wilaya Bunda Hoi, Serikali yawapa siku 30 Tu

Mradi Hospitali ya Wilaya Bunda Hoi, Serikali yawapa siku 30 Tu

0

Naibu Katibu Mkuu Dkt. Dorothy Gwajima akihojiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama juu ya sakata la kuchelewesha ujenzi huo.

 Mkuu wa Wilaya Bibi Lydia Bupili akitoa ufafanuzi juu ya mawasiliano

Baadhi majengo yanayo elezwa kutokamilika kwa wakati (Picha zote na Atley Kuni)

****************************************

Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI, Bunda

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa siku thelathini kuanzia Oktoba 05, 2019 kwa Halmashauri ya Wilaya Bunda mkoani Mara, iwe imekamilisha miradi yake yote yenye utata na ianze kutoa huduma kwa wananchi, ifikapo tarehe 25 Desemba, 2019. Dkt. Gwajima ameagiza pia jopo la wataalam kutoka OR-TAMISEMI kwenda wilayani humo kufanya ukaguzi maalum kwa miradi yote yenye utata.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo hivi leo wakati wa ziara yake kwenye mikoa ya Kanda ya ziwa ambapo alionekana kutoridhishwa na mwenendo wa miradi ya Halmashauri  husuani  ni ule wa Hospitali ya Wilaya ambao ulipokea fedha kiasi cha bilioni 1.5 toka mwezi Januari, 2019 lakini ujenzi wake ukaanza mwezi Mei, 2019 kutokana na malumbano baina ya viongozi wa eneo hilo.  

“Kwakweli mimi  ambaye nimepewa dhamana  yakusimamia sekta hii katika, mwendo huu hauniridhishi kabisa, jana nilikuwa Rorya, Umoja, Mshikamano na kutenda kazi kwa mshikamano nilio uona pale siuoni kabisa ndani ya Halmashauri hii ya Bunda” alisema Gwajima na kuongeza kwamba, “ninataka ndani ya siku 30 yaani mwezi mmoja kuanzia sasa Mkurugenzi, Miradi yote inayo lalamikiwa iwe imekamilika na taarifa tuipate TAMISEMI” aliagiza Gwajima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kusaja Amos, ilionesha, katika mwaka wa fedha wa 2018/19, Halmashauri ilipokea kiasi cha bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hata hivyo kutokana na malumbano baina ya viongozi hao, shughuli rasmi za ujenzi zikaanza  Mwezi Mei, 2019 na ilipofika tarehe 31 Juni,2019 fedha zote ambazo zilikuwa hazijaingia katika mpango wa manunuzi zilirejeshwa hazina kama sheria za fedha zinavyo elekeza.

Pamoja na Mkurugenzi kujitetea mbele ya Naibu Katibu Mkuu kuwa, ujemzi huo umefikia asilimia 70 ya ujenzi wote hali ni tofauti na uhalisia kwani hadi siku ya ziara baadi ya Majengo yaliwa ndio kwanza yanamwagiwa zege ili yaanze kunyanyuliwa.

“Mkurugenzi ukisema jingo limefikia asilimia 50, tutegemee kuona majengo yote yaliyoelekezwa yawe yamefunikwa na mmeanza umaliziaji, sasa wewe hapa ndio kwanza majengo takrinan manne ndio yameanza kupigwa paa na kuezekwa na jingo linguine ndio kwanza wanamwaga zege wewe unasema asilimia 70 huku sikuudanganya umma wa watanzania?” Alihoji Dkt. Gwajima.

Kufuatia kulalamikiwa kwa miradi mingi ya Halmashauri hiyo, ikiwapo ule wa ujenzi wa Ofisi ya Mbunge, Zahanati ya Namalabe pamoja na pamoja na kituo cha Afya Mugeta kilichopelekewa fedha kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu lakini hadi siku ya Ziara ya Naibu Katibu Mkuu kulikuwa na kasoro nyingi za kitaalam.

Katika Hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu akiwa katika ziara hiyo, amewaelekeza wakurugenzi  kote nchini kufanya sensa ya watumishi waliojiendeleza  kielemu na sasa wapo tayari kufanyiwa recategorization lakini bado wanasomeka kwenye miundo ya kizamani ilihali kimajukumu wameongezewa mzigo.

“Nitumie fursa hii nikiwa hapa katika kituo cha Nyasho, kupeleka salaamu zangu kwa Wakurugenzi na Maafisa Utumishi, wapitie na kufanya sensa kubaini watumishi wanaohitaji kubadilishiwa muundo, lakini kwa hila tu za Afisa  mtumishi huyo amekaa zaidi ya miaka saba hajabadilishiwa kazi lakini anapewa majukumu ya kazi mpya bila maslahi yake kuboreshwa” alikemea Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima yupo katika ziara ya ufatiliaji utendaji kazi na hali ya miundombinu ya Afya ambapo katika siku yake ya pili ametembelea na kukagua vituo cha Afya Nyasho na Makoko vyote vya  Musoma mjini, Hospitali ya Wilaya ya Musoma vijijini, Hospitali ya Wilaya Halmashauri ya Bunda  sambamba na Zahanati ya Mugeta.