Home Mchanganyiko TAEC NA IAEA YATOA MAFUNZO KWA WATAALAM KINGA NA UDHIBITI WA MIONZI

TAEC NA IAEA YATOA MAFUNZO KWA WATAALAM KINGA NA UDHIBITI WA MIONZI

0

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) katikati mwenye suti ya kijivu akiwa akiongea na watalamu wa kitaifa wa Kinga na Udhibiti wa mionzi kutoka katika nchi 23 za bara la AFrika waoaohudhuria mkutano huo unaofanyika jijini Arusha.
Wataalamu wa kitaifa wa kinga na udhibiti wa mionzi kutoka nchi 23 za bara la AFRIKA akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) mwenye suti ya kijivu mstari wa chini mara baada ya kufungua warsha ya siku tano ya majadiliano ya utekelezaji wa viwango vya kimataifa vya kinga na udhibiti wa mionzi vilivyotolewa mwaka 2014 na Shirika la kimaitaifa la Nguvu za Atomiki Duniani(IAEA)
………………

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) inaendesha warsha inayohusisha  wataalamu wa kitaifa wa kinga na udhibiti wa mionzi kutoka katika nchi 23 kutoka katika Bara la Afrika ambao ni wanachama wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani 

Lengo la warsha  hii ilionza hivi leo,  ni kujadiliana uzoefu wa nchi za Afrika zilizopata kutekeleza viwango vya kinga na udhibiti wa mionzi  vilivyotolewa mwaka 2014 na shirika la kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani na pia kujadili changamoto zilizowahi kujitokeza na kuzifanyia marekebisho.

Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Prof. Lazaro Busagala amewataka watalaamu hao kujadiliana na kutoa mapendekezo sahihi yatakayosaidia kuwakinga wananchi na  mazingira katika nchi zao dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi. 

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha mionzi katika Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) Bwana Tony Colgan amesema kuwa washiriki wa mkutano huo wanapaswa kujadiliana na kupata mbinu zitakazowezesha kuboresha ulinzi na usalama katika mionzi. Amesistiza kuwa IAEA inapenda