Home Mchanganyiko MAMLAKA ZA MAJI ZATAKIWA KUBUNI MIRADI YA KUPATA MIKOPO NA FEDHA ZA...

MAMLAKA ZA MAJI ZATAKIWA KUBUNI MIRADI YA KUPATA MIKOPO NA FEDHA ZA KUENDESHA MIRADI YA MAJI NCHINI

0

Naibu Katibu mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga akitoa hutoba yake leo kwenye Ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mamlaka za maji mikoa inayoendelea jijini Arusha ambapo amezitaka mamlaka hizo kutumia mafunzo hayo kuleta tija ya kuondoa uhaba wa maji nchini na kwa kujindesha badala ya kugemea ruzuku ya serikali

Afisa mtendaji mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mabomba ya plastiki ya maji Plasco Limited ya Dar es salaam akiongea na vyombo vya habari kwenye warsha ya siku tatu ya masuala ya jinsi ya kupata fedha za miradi midogo na mikubwa ya maji na kuwataka wadau hao kutumia fedha zao kidogo wanazokopa kununua biadhaa za hapa nchini

Sehemu ya maonyesho yaliombatana na warsha hiyo pichani ni mabomba ya maji yanayotengenezwa na Kampuni za kitanzania ya Plasco Ltd ya Dar es salaam kama yanavyoonekana

Pichani picha na Ahmed Mahmoud Arusha

……………………….

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wizara ya maji imezitaka mamlaka na wadau wa maji nchini kuhakikisha wanatumia ushirikiano na uzoefu wao kupata fedha na mikopo ya kujenga miradi ambayo itatoa huduma bora za maji kwa wananchi na kuacha tabia ya kuweka taarifa kwenye mafaili.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akifungua warsha ya siku tatu ya wadau wa maji kutoka mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na shirikisho la wasambazaji wa maji nchini (Atawas) jijini Arusha.

Alisema kuwa lengo kubwa la mafunzo ni upatikanaji wa fedha za miradi ya maji itakayowasaidia wananchi kupata huduma bora za maji safi na salama kwa bei nafuu kwa kuwatumia wadau wa taasisi za kifedha kupata mikopo ya ujenzi wa miradi midogo na mikubwa.

“Wakitoka hapa washiriki wote wahakikishe wanaenda kutekeleza kwa vitendo ili wananchi wapate huduma bora za maji za bei nafuu sio kwenda na kuandika taarifa ziishie kwenye mafaili tunataka utekelezaji wenye tija kwa maendeleo ya tasnia ya maji nchini”alisisitiza Sanga.

Alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano imejikita kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani hivyo kuwataka watendaji wote ndani ya wizara hiyo ziwemo mamlaka za maji mikoa kufanyakazi ya kutekeleza miradi kwa ubora kwa lengo la wananchi kupata huduma bora za maji ili kufanikisha azma hiyo ya serikali

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji ya plastiki (PLASCO LTD)Allimiya Osman alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikizalisha mabomba ya maji yenye uwezo mkubwa duniani katika kuhimili, kuhifadhi na kupitisha maji kwa muda wa mrefu bila kuharibika.

Alisema teknolojia inayotumika kutengeneza mabomba hayo inatumika kote duniani hivyo kuwataka wadau wa maji nchini kuhakikisha wanashirikiana na wadau hao wa maji katika kukambiliana na changamoto za maji katika kuboresha huduma za maji nchini.

Alisema kuwa ili kufanikiasha suala zima la utoaji huduma wanasisitiza serikali na wadau wa maji kuangalia matumizi ya fedha wanazopata kwa kununua bidhaa za viwanda vya hapa nchini ili kuongeza wigo wa mapato na kupunguza tatizo la ajira.

Awali akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi mwendeshaji wa taasisi ya wadau wa huduma za maji nchini (ATAWAS)Costantino Fidelis alisema kuwa uhaba wa maji unatokana na ukosefu wa fedha za ujenzi wa miradi ya maji ndio maana wameamua kuwajengea uwezo watendaji wa mamlaka za maji mikoa kupata mafunzo ya kuombea fedha za miradi kutoka kwenye taasisi za kifedha kutekeleza upatikanaji wa maji nchini
.
Alisema kuwa hayo ndio yamewafanya kuona umuhimu wa kuendesha warsha hiyo ili kuona miradi ya maji ikitekelezwa na kuondoa uhaba wa maji nchini ikiwemo kwenye suala zima la upatikanaji wa fedha kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani

“Matarajio ni kufungua milango kwa mamlaka za maji kuwa na fedha za kutosha kutekeleza miradi ya maji nchini ambayo itasaidia kuondoa uhaba wa maji kwa wananchi wengi zaidi hivyo kufikia malengo ya serikali” alisema Fidelis