Home Mchanganyiko BTI YAAGIZWA KUSHIRIKIANA NA HALMASHAURI KUTOA ELIMU YA UFUGAJI NYUKI

BTI YAAGIZWA KUSHIRIKIANA NA HALMASHAURI KUTOA ELIMU YA UFUGAJI NYUKI

0

Samwel Samumba  Stashahada ya Ufugaji nyuki mwaka  wa pili akitoa ufafanuzi wa matumizi ya mizinga ya kisasa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce  Nziku wakati wa maonesho jana ya ufugaji nyuki kwenye sherehe za mahafali ya nane ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora.

Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za mahafali ya nane ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku akitoa hotuba jana wakati wa mahafali ya nane ya Chuo cha Mafunzo ya ufugaji Nyuki Tabora.

Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii  Dkt. Aloyce Nziku (katikati) akishirikiana na Vijana wa Msange  JKT kuimba wimbo maalumu wakati wa sherehe za mahafali ya nane ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora jana

***********************************

NA TIGANYA VINCENT

CHUO cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora kimetakiwa kushirikiana na Halmashauri mbalmbali ili kuhakikisha kinaifanya sekta ya ufugaji nyuki inatoa mchango na kuwa kichocheo kikubwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku wakati wa mahafali ya nane ya Chuo hicho mjini Tabora.

Alisema ni vema Chuo kihakikishe wa wafugaji nyuki wengi wanapata elimu ili waweze kutumia mbinu za kisasa za uzalishaji wa asali kwa ajili ya kuongeza ubora unaotakiwa na uzalishaji wa asali nchini.

Dkt. Nziku alisema ufugaji wa nyuki hautaji matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya kununulia dawa kama zile za mifugo wengine za kukabiliana na magonjwa bali anachohitaji ni kuwa na eneo la msitu na mizingi iliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ili kuongeza uzalishaji na ubora wa asali.

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wahitimu wa mafunzo ya ufugaji nyuki kutumia elimu waliyopata kwa kujiari wenye kwa kuanzia mashamba darasa ya ufugaji nyuki na uzalishaji asali wa kitalaamu.

Alisema hatua itawasaidia kuepuka lawama za kutokuwa na ajira kwa kuwa chanzo kizuri cha mapato ambayo yatawapelekea kupata fedha nyingi.

 “Mwajiriwa Serikalini atasubiri miaka thelathini ifike ndipo alipwe mafano yake ambayo yaweza kuwa milioni 300 au 500 ,lakini mtu aliyejiari mwenyewe fedha hiyo anaweza kuipata kwa muda mfupi” alisema.

Aliwataka wahitimu kuangalia fursa za kuanzisha vikundi na kuwa na andiko ambalo litawasaidia kupata mikopo ambayo itawawezesha kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki.

Dkt. Nziku aliongeza kuwa hatua itasaidia sio tu kupata faida bali kutoa utaalamu wa ufugaji nyuki na uhifadhi wa mazingira kwa wananchi wengi na kuwafanya waone kuwa nyuki ni rasilimali nyuki kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora Semu Daudi alisema kuwa wanatarajia kutumia msitu wa Simbo uliopo wilayani Uyui kama shamba darasa ili kuwafikia wananchi wengi wanaohitaji mafunzo  hayo.

Katika mahafali hayo ya nane ya Chuo hicho jumla ya wahitimu 116 wamehitimu mafunzo ya ufugaji nyuki ambapo astashahada ni 61 na shahada ni 54.