Home Mchanganyiko JAFO AAGIZA UONGOZI WA JIJI LA DODOMA KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE YA...

JAFO AAGIZA UONGOZI WA JIJI LA DODOMA KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE YA MSINGI MFANO NOVEMBA 30,2019

0

Afisa Elimu Msingi Halmashauri jiji la Dodoma Charles Mabeho, Akisoma taarifa kwa Waziri wa Tamisemi Mhe.Selemani Jafo wakati wa ziara ya kikagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Mfano iliyopo Kata Ipangala jijini Dodoma.

Waziri wa Tamisemi Mhe.Selemani Jafo ,Akitoa maelezo kwa Uongozi wa jiji la Dodoma wakati wa ziara ya kikagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Mfano iliyopo Kata ya Ipangala jijini Dodoma.

********************************

Na. Alex Sonna, Dodoma 

Serikali imeutaka Uongozi wa Halmashauri ya jiji la Dodoma hadi kufika Novemba 30,mwaka huu uwe umekamilisha ujenzi wa shule mpya ya msingi Mfano iliyopo Kata ya Ipagala.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Mfano.

Mhe. Jafo amesema kuwa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi huo kutokamilika kwa muda huku wakidai fedha za ujenzi zimekwisha na kutaka kuongezewa kiasi cha shilingi 241,931,126.40.

“ Siwezi kuwaelewa mkinambia ujenzi huu haujakamilika na mnataka fedha zaidi wakati mlipewa kiasi cha shilingi 706,400,000 na wenzenu wameshakamilisha kwa kupitia fedha hizo na shule zao  zimeshaanza kufanya kazi” amesisitiza Jafo.

Aidha Jafo amesema kuwa uongozi wa jiji hilo watafute fedha sehemu yoyote ilimradi kukamilisha ujenzi huo kwa muda unaotakiwa kwani hawezi kutoa fedha nyingine kama hapo awali alivyoomba Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma Charles Mabeho katika taarifa yake aliyoisoma mbele ya Waziri Jafo.

Hata hivyo ametoa wito kwa uongozi huo kuhakikisha na kusimamia ujenzi ili uweze kukamilika kwa muda unaotakiwa na uwe katika ubora unaoendana na kiasi cha fedha zilizotolewa na Serikali. Ameseama Mhe.Jafo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amekiri kuwa timu yake ya uongozi imeteleza katika utekelezaji wa ujenzi huo ila kupitia muda waliopewa na Waziri  watajipanga vyema ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika katika ubora unao hitajika na kuendana na gharama za fedha zilizotolewa na Serikali.

Awali Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya jiji la Dodoma Charles Mabeho akisoma taarfa ya ujenzi huo amesema kuwa walipokea kiasi cha shilingi 706,400,000 katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.