Home Mchanganyiko RC MAKONDA AFANIKISHA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 500 WENYE TATIZO LA...

RC MAKONDA AFANIKISHA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 500 WENYE TATIZO LA MOYO KWA KIPINDI CHA MWAKA MZIMA, NI WALE WALIOFANYIWA UPASUAJI NA WANAHITAJIKA KUHUDHURIA CLINIC LAKINI HAWANA UWEZO WA KIFEDHA.

0

********************************************

Ubalozi wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE umeendelea kuunga mkono kampeni ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto kutoka familia duni Iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Makonda ambapo leo October 31 wamemkabidhi hundi ya Shilingi Milioni 27 kwaajili ya Bima za Afya kwa Watoto 500 wenye Tatizo la Moyo.

RC Makonda amesema kiasi hicho cha fedha kitawezesha Watoto 500 wakiwemo yatima na Wanaotokea familia duni Waliolazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kupata Bima za Afya zitakazowawezesha kupata Matibabu Bure kwa kipindi cha Mwaka Mzima.

Aidha RC Makonda amesema uamuzi wa kuwatafutia Bima za Afya umekuja baada ya kubaini Watoto wengi wanaofanyiwa upasuaji wanahitajika kwenda Clinic kwaajili ya kufuatilia maendeleo ya Afya na Dawa lakini kutokana ugumu wa maisha wanashindwa kumudu gharama jambo linalowafanya Wazazi au Walezi wao kuuza Mali walizochuma kwa muda mrefu ili wapate fedha na mwisho wa siku familia inazidi kuwa maskini.

Pamoja na hayo RC Makonda amemshukuru Balozi kwa kuendelea kumuunga mkono katika mambo mbalimbali ikiwemo kusomesha watoto 100 wa kike kidato cha tano na sita, Kumpatia madaktari bingwa wa Moyo Waliofanya upasuaji kwa watoto 60, Kumsaidia futari kwaajili ya Maimamu wa Misikiti 800 huku akitoa wito kwa Wananchi kuwa na moyo wa upendo wa kusaidia wenye uhitaji.

Kwa upande wake Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu Bw. Khalifa Abdulrahman Almarzooqi amesema kuwa Ubalozi huo unafurahishwa na kazi nzuri ya RC Makonda katika kusaidia Wananchi wenye uhitaji ndio maana wameamua kushirikiana nae kwa kila jambo kwakuwa kila msaada anaoupokea unawafikia walengwa.