Home Siasa UVCCM IRINGA: WASAKA UBUNGE KWA NJIA YA RUSHWA KUKIONA CHA MTEMA KUNI

UVCCM IRINGA: WASAKA UBUNGE KWA NJIA YA RUSHWA KUKIONA CHA MTEMA KUNI

0

 Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm (UVCCM) mkoa wa
Iringa Kenani Kiongosi akiwana baadhi ya viongozi wa UVCCM mkoa wa Iringa pamoja na wadau wa chama cha mapinduzi Mkoa wa iringa   
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
MWENYEKITI wa umoja wa vijana wa
ccm (UVCCM) mkoa wa Iringa Kenani Kiongosi amewataka wanasiasa mbalimbali
wanaousaka ubunge wa jimbo la Iringa Mjini  kufuata misingi ya chama ili wapite kwenye
kanuni na taratibu za chama.
 
Akizungumza na viongozi wa
UVCCM mkoa wa Iringa Kihongosi alisema kuwa viongozi wote wanaoutafuta ubunge
katika jimbo la Iringa mjini wanatakiwa kufuata utaratibu unatakiwa na chama
cha mapinduzi ili kumpata kiongozi bora.
 
“Katika kipindi cha miaka kumi
sasa tumekuwa tukipoteza jimbolaIringa mjini kwa kuwa na makundi kutokana na
viongozi warafi na waroho wa madaraka kwakutoa rushwa kwa wapiga kura ili
waweze kupata ubunge,kwa sasa hatuwezi kukubali swala hilo kwa kuwa
tunahujumiwa kutokana na makundi ambayo yamekuwa yakitokeza kipindi cha
uchaguzi” alisema Kihongosi
 
Kihongosi alisema kuwa kumekuwa
na viongozi wanaoutaka ubunge Iringa Mjini wameanza kufanya kazi wanavyojitakia
wao bilakufuata njia sahihi ambazo zinatakiwa,badala yake wamekuwawakitoa fedha
kwa baadhi ya wadau kwa lengo la kutengeneza makundi ambayo hayana faida kwa
wananchi wa Manispaa ya Iringa.
 
Aidha Kihongosi aliwataka
vijana wa chama cha mapinduzi kukataa mara moja kutumika kuwa daraja kuwatafutia
ubunge viongozi ambao hawana msaada katika jumuiya katika kuleta maendeleo kwa
vijana ambao ndio wamekuwa wakitumia kuleta ushindi kwamgombea wa chama cha
mapinduzi.
 
“Vijana acheni mara moja kutumika
kwa viongozi wasaka tonge ambao wamekuwa wakipata madaraka hawakumbuki mchango
wa vijana wakati wa kukitafuta cheo chake”alisema Kihongosi
 
Kihongosi alisema mwaka 2015
kulikuwa namakundi makubwa mawili ambayo yalikuwa katika ya wenyeviti na
makatibu na kupelekea kupoteza jimbo la Iringa Mjini na kulikuwa na mvurugano mkubwa
kweli ambao ulimpa tena ubunge Mchungaji Petter Msigwa.
 
“Nitasikitika sana kuona kijana
mmoja ambaye ni kiongozi kumbeba mgombea furani,nikikutambua mapema
nitakupeleka kwenye kamati husika na tutakuondoa kwenye nafasi ambayo uponayo
hivi sasa ili usituvuruge kwenye harakati zetu za kulikomboa jimbo la Iringa
Mjini” alisema Kihongosi