Home Michezo “VAR” JINI LINALOJIGEUZA KUWA MALAIKA NA KUPOTEZA LADHA YA MCHEZO

“VAR” JINI LINALOJIGEUZA KUWA MALAIKA NA KUPOTEZA LADHA YA MCHEZO

0
Imani Kelvin Mbaga,Dar es Salaam

Kama kuna gumzo kubwa duniani siku hizi hasa baada ya michezo ya ligi mbalimbali huko ulaya ni mamaamuzi “tata” yanayotokana na teknolojia mpya ya “muamuzi msaidizi kwa kutumia video” au “var” kama inavyofahamika na wengi.

Ghafla baada ya utambulisho wa teknolojia hii, imegeuka kuwa “nyota wa mchezo” mara nyingi sana, ikiokoa wengine na kuzamisha wengine.

Teknolojia hii ilitambulishwa ili kuondoa utata wa maamuzi hasa katika matukio muhimu yanayohitaji kutolewa uamuzi sahihi ama kwa sababu ya uharaka wa ufanyikaji wa tukio husika au ufinyu utokanao na umbali wa tukio husika toka kwa waamuzi.


Lengo la teknolojia hii ni kumuwezesha muamuzi kufanya MAAMUZI sahihi katika baadhi ya matukio kama vile rafu na kuotea ili aweze kutoa adhabu stahiki kama kadi, pigo dogo au kubwa nk.
Lengo la “var” ni kuondoa ubinadamu katika mchezo wa mpira na kuleta usahihi wa maamuzi kwa asilimia mia moja.


Kwa mujibu wa takwimu za FIFA “var” imefanikiwa kwa zaidi ya 90% kuondoa utata na kwa mantiki hiyo “wamefanikiwa”.


Kwa sababu namba hazipingwi basi siwezi kupingana nao katika hilo, lkn napingana na mtizamo.


Nilianza kuiona “var” ikitumika kwenye ligi mbili moja Seria A na pili Bundesliga, ambapo niliichukia moja kwa moja teknolojia hii.
Sababu zangu za kuichukia ni mbili kubwa, moja ni kuondoa ladha ya mchezo wenyewe, linafungwa goli mnaogopa kushangilia hadi waamuzi wajiridhishe. Hakuna wakati mtamu kwenye soka kama wakati wa kunyanyuka kwenye kiti kushangilia au “kukaanga chips” “aaaaaah” mkiwa mmekosa goli.


Pili naichukia kwa sababu tunaondoa ubinadamu huku tukiwaachia binadamu waamue.

Yaani unataka kupunguza makosa ya kibinadamu lkn unasahau ni binadamu hao hao wanaotofautiana kimtizamo, tafsiri na hata uelewa ndiyo watakao tumia picha za marejeo wakiwa na akili zilezile, mitazamo ile ile nk ili kufanya maamuzi.Na ndiyo sababu tumeacha kujadili waamuzi tunajadili “VAR”, mpira bila “utata” hauna ladha