Home Mchanganyiko RC MNYETI AFAGILIA MIAKA MINNE YA RAIS MAGUFULI 

RC MNYETI AFAGILIA MIAKA MINNE YA RAIS MAGUFULI 

0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amefagilia miaka minne ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli kuwa ni ya maendeleo makubwa kwa wananchi wa Tanzania. 
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Maghagh Wilayani Mbulu, Mnyeti alisema miaka minne ya utawala wa Rais Magufuli imekuwa na mafanikio makubwa ya maendeleo. 
Alisema miaka minne ya Rais Magufuli imekuwa faraja kwa watanzania wengi ikiwemo miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo imebadili maisha ya Watanzania. 
Alisema maendeleo mengi yamefanyika nchini ikiwemo vituo vya afya, hospitali za wilaya, kuboresha elimu, maji, ujenzi wa barabara na ununuzi wa ndege. 
“Kwa maendeleo haya ya miradi mbalimbali ya maendeleo hivi tutamsahau Rais Magufuli, tunachopaswa kufanya ni kumpa zawadi ya ushirikiano na kumuombea kwa Mungu,” alisema Mnyeti. 
Alisema wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yao ya maendeleo binafsi na kwa jamii kwa ujumla. 
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Simbalimile Mofuga alisema miaka minne ya utawala wa Rais Magufuli yamefanyika maendeleo mengi mithili ya miaka 40.
Mofuga alisema Rais Magufuli amekaa madarakani miaka minne pekee lakini maendeleo yaliyofanyika kwenye utawala wake utadhani ametawala miaka 40.
Diwani wa kata ya Endamilay, Gesso Bajuta alisema maendeleo mengi yamefanyika wilayani Mbulu kipindi cha Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya. 
“Majengo makubwa ya hospitali mpya kwa shilingi bilioni 1.5 ni maendeleo makubwa mno yamefanyika tunamshukuru sana Rais Magufuli,” alisema Bajuta