Home Mchanganyiko MKURABITA YATAKIWA KUHAKIKISHA HATIMILIKI ZA KIMILA ZINATUMIKA KUWAPATIA MIKOPO WANUFAIKA WA MPANGO...

MKURABITA YATAKIWA KUHAKIKISHA HATIMILIKI ZA KIMILA ZINATUMIKA KUWAPATIA MIKOPO WANUFAIKA WA MPANGO HUO ILI WAJIENDELEZE KIUCHUMI

0

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika mkoa wake jana kabla ya Naibu Waziri huyo kuanza ziara ya kikazi mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba na Tunduma mkoani Songwe jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)na kuzungumza na watumishi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Ardhi, Bw. Kelvin Joseph alipokuwa akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa maelekezo ya namna ya kuwaunganisha wanufaika wa MKURABITA na taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo na kujiinua kiuchumi wakati Naibu Waziri huyo aliposimama kukagua utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe katika ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanufaika wa  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango huo.

***************************************

Aaron Mrikaria-Songwe

Tarehe 25 Oktoba, 2019

Watendaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wametakiwa kuratibu taasisi za fedha
zenye utayari wa kuwapatia mikopo wanufaika wa Mpango huo wenye
hatimiliki za kimila ili waweze kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi
zitakazowawezesha kuinua kipato na kuboresha maisha yao.

Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua utekelezaji wa
Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania (MKURABITA).

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya wanufaika
wa Mpango huo katika Kijiji cha Naming’ongo ambao wamesema
wanashindwa kutumia hatimiliki za kimila kupata mikopo kutokana na
kukosa mwongozo na utaratibu wa upatikanaji wa mikopo kwenye taasisi
za fedha, licha ya hatimiliki hizo kupunguza migogoro ya ardhi.

“Nawapa wiki mbili mnipe majibu ya taasisi za fedha zitakazokubaliana na
Serikali kutoa mikopo kwa kutumia hatimiliki za kimila, na kuongeza kuwa
elimu kwa umma itolewe ili wananchi waliorasimishiwa mashamba na
maeneo ya biashara wajue taratibu za kupata mikopo kwenye taasisi za
fedha zilizo tayari kutoa mikopo hiyo,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza Watendaji wa MKURABITA
kuharakisha zoezi la kutoa hatimiliki za kimila kwa wananchi
waliorasimishiwa ardhi, ikizingatiwa kuwa mchakato wa zoezi hilo huishia
wilayani hivyo hakuna sababu ya ucheleweshaji.

“Kama mwananchi ameshatekeleza taratibu zote za urasimishaji, kuna haja
gani ya kusumbuliwa wakati upatikanaji wa hatimiliki za kimila ni
makubaliano ambayo yanakamilika katika ngazi ya kijiji na si wizarani,”
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa alipata fursa ya kuona mashamba ya mpunga
ya wanufaika wa MKURABITA wa Kijiji cha Naming’ongo na kuwapongeza kwa kilimo cha kisasa.

Jumla ya mashamba 776 yamerasimishwa katika Halmashauri ya Wilaya
ya Momba mkoani Songwe ambapo kati ya hayo, hatimiliki za kimila 527
zimeshatolewa.