Home Mchanganyiko UZINDUZI WA HUDUMA YA TIBA YA DIALYSIS KATIKA HOSPITALI KUU YA JESHI...

UZINDUZI WA HUDUMA YA TIBA YA DIALYSIS KATIKA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

0

**********************

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika jitihada za kuboresha huduma ya Afya linatarajia kuzindua Idara mpya ya huduma ya Tiba ya Dialysis katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo.

Shughuli za uzinduzi huo zinatarajia kufanyika kesho Jumatano tarehe 23 Oktoba, 2019 kwenye Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo iliyopo Jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili na nusu (2:30) asubuhi. Mgeni rasmi katika shughuli hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Ukiwa mdau katika Tasnia ya Habari, JWTZ linakialika chombo chako cha Habari kwenye hafla hiyo muhimu ili kuuhabarisha umma juu ya huduma hiyo kupatikana Jeshini.