Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Leonard Akwilapo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu mashindano ya kitaifa ya michezo na Sanaa kwa vyuo vya Ualimu Tanzania bara yatakayofanyika mkoani Mtwara kuanzia Oktoba 25,Mwaka huu.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG
……………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MASHINDANO ya kitaifa ya michezo na sanaa kwa Vyuo vya Ualimu Tanzania bara(UMISAVUTA), yanatarajia kuanza kutimua vumbi mkoani Mtwara Oktoba 25, mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Leonard Akwilapo,amesema kuwa mashindano hayo yatachukua siku sita Oktoba 25 hadi 31, mwaka huu na yatajumuisha zaidi ya washiriki 5,600 kutoka vyuo vya ualimu vya serikali 35.
Ufunguzi wa mashindano hayo utafanyika Oktoba 27 katika uwanja wa Nagwanda Sijaona mkoani Mtwara huku mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye atakuwa anamwakilisha Waziri Mkuu.
Mashindano hayo yatajumusiha michezo mbalimbali kama vile mpira wa pete, miguu, wavu, kikapu, riadha na pia mashindano ya uchoraji, sanaa za maonesho, ngoma na kwaya.
” Hivyo tunaamini mashindano haya yataleta chachu na hamasa kubwa na kuwaomba walimu wawe na weledi kufundisha masomo ya sanaa na michezo”amesema Dk.Akwilapo
Aidha Dk.Akwilapo ameipongeza timu ya Tanzania ‘Taifa stars’ kwa kufanikiwa kufuzu fainali za mashindano ya mataifa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani(CHAN) yatakayofanyika mwakani nchini Cameroon.