MKUU wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akimkabidhi kitabu cha mongozo wa mawasiliano kwa mwananchi aliyetembelea maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa pwani yanayofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa.
Afisa Mwandamizi wa Mitambo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki Kenneth Chitemo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TCRA katika maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani yanayofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akiwa picha pamoja na wadhamini wa maonesho ya viwanda.
Wakuu wa Taasisi wakiwa katika Kongamano la wiki ya viwanda mkoa wa Pwani yanayofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
*****************
Na Mwandishi WETU
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imeshiriki maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani katika utoaji wa elimu ya mawasiliano pamoja na usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
Akizungumza katika maonesho hayo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa katika maonesho hayo wananchi watembelee banda la TCRA kuweza kupata elimu namna ya kutumia l simu katika kupata maendeleo ya Taifa.
Mhandisi Odiero amesema kuwa uchumi wa viwanda unakwenda na mawasiliano ya simu na kutaka wadau kutumia simu katika biashara zao kwa kutangaza biasha kwa kutumia simu hizo.
Aidha amesema TCRA iko katika kampeni ya kuhamasisha wananchi kujisajili kwa laini za simu kwa lama za vidole kwa muda uliopangwa na usajili huo utafungwa Desemba 31 mwaka huu.
“Tunataka wananchi wajisajili simu zao kwa alama za vidole kwa muda uliopangwa na wasije wakapata usumbufu wakati zoezi hilo likiwa limefungwa kwa laini za simu kutopata mawasiliano.amsesema Mhandisi Odiero.
Mhandisi Odiero amesema kuwa Kanda ya Mashariki ya TCRA itapita Wilaya zote zilizo katika kanda hiyo katika kutoa elimu ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja na huduma nyinginezo za bidhaa za mawasiliano.
Hata hivyo amesema kuwa wananchi waepuke kufanya maawsiliano na watu wasiowajua kwa kuwaomaba fedha ni mpaka pale watakapojiridhisha na katika mawasiliano kwani baadhi yao wanafanya utapeli.