**********************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkutano wa Sadc ambao unaendelea umebeba madhumuni ya kuangalia mwenendo mzima wa hali ya mazingira na mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni pamoja na kubainisha utekelezaji wa mikakati ya hifadhi ya usimamizi wa mazingira
Mkutano huo kesho utaingia hatua ya pili ya makatibu wakuu baada ya wataalamu kumaliza ngwe yao jana na utafunguliwa na Waziri mwenye dhamana ya utalii Dkt.Khamis Kigwangalah kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa Aicc jijini hapa
Kwa mujibu wa Taarifa kwa vymbo vya habari iliyotolewa kwa wanahabari juzi na Naibu Msemaji wa Serikali Zamaradi Kawawa alisema kuwa watapitia mkakati wa SADC wa uchumi wa bahari na kutathmini maendeleo katika sekta za misitu wanyamapori na utalii.
Alisema kuwa mkutano huo unakuja baada ya serikali ya Tanzania kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika inayojumuisha nchi 16 na Tanzania ndio mwenyekiti wa jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka moja.
Alisema mkutano huo ni sehemu ya majukumu ya uwenyekiti wa Nchi yetu chini ya mwenyekiti wake kwa sasa Rais Dkta John Magufuli na kikao cha makatibu wakuu kitafunguliwa kesho tareh 21 na Waziri wa maliasili na utalii Dkt Khamisi Kigwangallah ikiwa ni sehemu ya kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa kwenye kikao cha mawaziri.
Kikao cha mawaziri ambacho kitafanyika tarehe 25 oktoba kwenye ukumbi huo huo wa AICC jijini Arusha na utafunguliwa na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ambapo Tanzania ni miongoni mwa wananchma wanaotekeleza mkakati wa SADC kuhusu usimamizi wa sheria na vita dhidi ya Ujangili wa wanyamapori.
Aidha mkutano huo pia utajadili masuala mbali mbali ya kuboresha mistu ikiwa ni pamoja na masuala ya mazingira maliasili utalii na kubwa ni mabadiliko ya kimazingira na ujangili unaovuka mipaka