Home Michezo MANCHESTER UNITED, LIVERPOOL WATOSHANA NGUVU

MANCHESTER UNITED, LIVERPOOL WATOSHANA NGUVU

0

*******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Moja ya klabu ya jijini Manchester, Manchester United imeambulia sare dhidi ya klabu ya Liverpool katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza ambapo matokeo yalikuwa 1:1.

Manchester United walianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Marcus Rashford mnamo dakika ya 36 na kumuacha kwenye mataa mlinda mlango Allison.

Sadio Mane alipachika bao la kusawazisha dakika ya 43 teknolojia ya VAR ilikataa bao hilo kwa kuwa uligusa mkono kabla ya kuzama wavuni.

Iliwabidi Liverpool isubiri mpaka dakika ya 85 walipopachika bao kupitia Adam Laliana na kuweka mzani Sawa.

Liverpool inasalia kileleni ikiwa na pointi 25 huku Manchester United ikiwa nafasi ya 10 na pointi zake 10.