Home Mchanganyiko KIWANDA CHA CHUMVI GEREZA KIWANDA CHUMVI MTWARA KUBORESHWA

KIWANDA CHA CHUMVI GEREZA KIWANDA CHUMVI MTWARA KUBORESHWA

0

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiagana na Mkuu wa Wilaya Newala, Mhe.Aziza Mwanwasongo alipomtembelea Ofisi kwake kwa mazungumzo katika ziara yake ya kikazi Wilayani Newala, Mkoani Mtwara(Picha na Jeshi la Magereza).

Askari wa Gereza Kuu Lilungu wakiwa timamu katika Paredi wakati Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipowasili katika viwanja vya gereza hilo leo Oktoba 17, 2019 katika ziara yake ya kikazi.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiangalia chumvi ambayo ipo tayari kwa matumizi katika ghala la kuhifadhia chumvi la Gereza Kiwanda Chumvi Mtwara alipotembeleakatika ziara yake ya kikazi leo Oktoba 17, 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua shamba la chumvi la Gereza Kiwanda Chumvi Mtwara pamoja na sehemu ya mkondo wa maji ya bahari ambapo hivi karibuni mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo hayo ya Gereza ziliharibu kingo za mashamba ya chumvi.

Sehemu ya matofali ya saruji ambayo yatatumika katika ujenzi wa nyumba za makazi ya askari katika Gereza Kuu Lilungu. Pichani ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua tofali hizo.

***************************

Na ASP. Lucas Mboje, Mtwara

JESHI la Magereza lina mpango wa kukiboresha Kiwanda chake cha uzalishaji chumvi katika Gereza Kiwanda Chumvi Mtwara ili kupanua shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho kilichopo Mkoani Mtwara.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ameelezea adhima hiyo leo Mkoani Mtwara wakati akizungumza na uongozi wa Gereza hilo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Jeshi hilo.

Amesema kuwa kiwanda hicho lazima kiboreshwe kwa kuwekewa miundombinu mizuri ili kukidhi mahitaji halisi ya soko la chumvi hapa nchini.

“Mradi huu wa uzalishaji chumvi ni fursa kubwa ndani ya Jeshi letu hivyo ni lazima tukiboreshe kwa kukijengea miundombinu mipya pamoja na kufanya maboresho ya shughuli za uzalishaji wa chumvi ili kuongeza uzashaji,” amesisitiza Jenerali Kasike.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike ameupongeza Uongozi wa Gereza Kuu Lilungu kwa kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais kuhusu kutatua changamoto ya makazi ya askari ambapo gereza hilo tayari limefyatua matofali 7,600 ya saruji pamoja na matofali ya kuchoma 25,000 ambayo yatatumika kujengea nyumba za watumishi wa Jeshi hilo.

“Nitumie fursa hii kumpongeza sana Mkuu wa Gereza Lilungu pamoja na maeneo mengine ya magereza yetu kwa mwitikio mzuri wa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli katika kutatua changamoto hii ya uhaba wa makazi ya askari,” Amesema Kamishna Jenerali Kasike.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kiwanda cha Gereza Chumvi Mtwara, SP. Wambura Kitoka amesema kuwa kiwanda hicho kinao uwezo wa kuzalisha chumvi ambayo inaweza kulisha magereza yote nchini ikiwa miundombinu ya uzalishaji itaboreshwa na kwa sasa kiwanda hicho kinao uwezo wa kuzalisha tani 300 za chumvi.

“Hivi sasa kiwanda chetu kinao uwezo wa kuzalisha tani 300 za chumvi, aidha malengo yetu nitani 700 za chumvi,” Amesema SP. Wambura.

Aidha, Mkuu huyo wa Kiwanda ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo uchakavu wa miundombinu pamoja na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo kunyesha kwa mvua kubwa hali ambayo inawaletea changamoto kubwa katika uzalishaji wa chumvi.

Gereza Kiwanda chumvi Mtwara lilianzishwa mwaka 1975, lina eneo lenye ukubwa wa ekari 265 na shughuli kubwa zinazofanywa na Gereza hilo ni mradi wa uzalishaji wa chumvi.