Mtaalamu wa Upishi wa bia wa TBL Group, Andrew Mugasha, akifafanua jambo juu ya upishi wa bia kwa wafanyabiashara hao na wamiliki wa bar jijini Dar es Salaam wakati walipotembelea katika kiwanda cha Bia cha Ilala jijini Dar es Salaam.
Mdhibiti wa Ubora wa Bidhaa wa TBL, Raymond Nkambi,akitoa somo la ubora wa Bidhaa kwa wafanyabiashara hao.
Mtaalamu wa afya na Usalama mahali pa kazi wa TBL , Anneth Mkuka akiongea na ujumbe wa wafanyabiashara hao.
Wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda
Picha ya pamoja ya Baadhi ya wafanyabiashara hao na maofisa wa TBL
………………..
Katika kuhakikisha inaenda sambamba na wadau wake mbalimbali, Kampuni ya kutengeneza bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL), imeandaa mpango wa wadau wake wanaouza bidhaa zake kutembelea viwanda vyake na kujionea na kujifunza mchakato mzima wa utengenezaji wa bidhaa zake.
Mbali na programu hii, TBL imekuwa na programu mbalimbali shirikishi za wafanyabiashara inaoshirikiana nao na wateja wake, kama ambavyo imekuwa ikiendesha programu yak kuwapatia elimu yak ujasiriamali wenye mabaa na mameneja wao ijulikanayo kama Retail Development Programme (RDP).
Baadhi ya wafanyabiashara waliofanya ziara katika kiwanda cha TBL cha Ilala, wameeleza kuwa wamefurahishwa na mpango huo na wameweza kujifunza bia zinavyozalishwa na kuona mitambo ya kisasa inavyofanya kazi sambamba na jinsi kampuni inavyozingatia ubora wa bidhaa zake kuhakikisha wateja wake wanapata bidhaa zenye ubora wa kiwango cha kimataifa.