Home Mchanganyiko WAZIRI BITEKO AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUJADILI CHANGAMOTO ZA MAKAA YA MAWE

WAZIRI BITEKO AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUJADILI CHANGAMOTO ZA MAKAA YA MAWE

0

Viongozi wa Makampuni ya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics
Company pamoja na Lake Cement Ltd wakimsikiliza Waziri wa Madini
Doto Biteko walipokuwa wakijadiliana changamoto za bei ya Makaa ya
Mawe jijini Mwanza.

Waziri wa Madini Doto Biteko akisalimiana na Viongozi wa makampuni
ya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake
Cement Ltd.

Waziri wa Madini Doto Biteko akiwafafanulia Viongozi wa makampuni ya
Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement
Ltd kuhusu utaratibu wa bei za Makaa ya Mawe.

Waziri wa Madini Doto Biteko akiwasikiliza Viongozi wa makampuni ya
Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement
Ltd, kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza Fredy Mahobe.

****************************

Na Tito Mselem, Mwanza

Waziri wa Madini Doto Biteko amewatoa wasiwasi Wawekezaji wa
Viwanda vinavyotumia Makaa ya Mawe na kuieleza Kampuni
inayochimba Makaa ya Mawe ya TANCOAL kuwa hairuhusiwi kuongeza
bei kiholela badala yake inatakiwa kuuza kulingana na bei elekezi
iliyopangwa na serikali.

Kauli hiyo ilitolewa Septemba 15, 2019 na Waziri Biteko baada ya
kukutana na wawekezaji wa Viwanda vya Saruji na Vigae kujadili
changamoto za Makaa ya Mawe katika kikao kilichofanyika katika Ofisi
ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza.

Katika Kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Biteko, kilihudhuriwa pia na
Mkurugenzi wa huduma za Leseni wa Tume ya Madini Mhandisi,
Yahaya Samamba, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza Fredy
Mahobe, Afisa Kodi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Venance Kasiki pamoja
na wawekezaji wa viwanda vya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics
Company pamoja na Lake Cement Ltd.

Kampuni hizo tatu za Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company
pamoja na Lake Cement Ltd. zinatumia kiasi kikubwa cha Makaa ya
Mawe kwa matumizi ya kuyeyushia Mawe kwa ajili ya uzalishaji wa
saruji na vigae ambapo zaidi ya nyuzi joto 2000 zinatakiwa ili kuyeyusha
Mawe hayo ziliomba kukutana na Waziri wa Madini ili kueleza
changamoto zao.

Hatua hiyo ilikuja kutokana na wanunuzi wakubwa wa makaa yam awe
nchini kuwa na mvutano wa bei ya Makaa ya Mawe kati yao na
mzalishaji wa Makaa hayo kampuni ya TANCOAL anayozalisha Mawe
hayo katika eneo la Kitai Mkoani Ruvuma katika Mgodi wa Ngaka.

Mvutano huo ulianza mara baada Serikali kupitia Tume ya Madini
Kuitaka Kampuni ya TANCOAL Kulipa deni lake la kiasi cha shilingi
Bilioni 23.9 ambazo zilitokana na malimbikizo ya kutolipa mrabaha wa
mauzo na usafirishaji wa Makaa hayo pamoja na adhabu ya asilimia 50
kuanzia Septemba 2011 mpaka Juni 2019.

Aidha, Waziri Biteko amezitaka kampuni hizo kuendelea na uzalishaji wa
Saruji na Vigae bila kuhofia kupandishiwa bei kwa maana bei hazitapanda kiholela, ameeleza kuwa, Makaa ya Mawe kote nchi yatauzwa kulingana na bei iliyo elekezwa na serikali.

Imeonekana kwamba, deni la kampuni ya TANCOAL kuwa kubwa,
kampuni hiyo imeonesha nia ya kupandisha bei kwanye Makaa ya
Mawe ili kufidia deni wanalodaiwa na Serikali.

Kwa upande wake, Mdhibiti wa Fedha wa Tanga Cement, Issac
Lupokela alimweleza Waziri Biteko kuwa, kitendo cha kupandishiwa bei
na kampuni ya TANCOAL ni kama wanawaadhibu kutokana na ukweli
kwamba hakuna mbadala wa kununua kwa wingi sehemu ingine makaa
hayo baada ya serikali kusitisha uingizwaji wa Makaa ya Mawe nchini.

“Kipindi cha Nyuma tulikuwa tunanunua Makaa ya Mawe kutoka Afrika
ya Kusini kwa kuwa Makaa yaliyokuwa yanazalishwa nchini hayakuwa
na kiwango cha kutosha hivyo baada ya serikali kusitisha uingizwaji wa
Makaa ya Mawe nchini, tulilazimika kushirikiana na kampuni ya
TANCOAL ili kutoa elimu ya namna bora ya uzalishaji wa Makaa hayo,
leo tunashangaa wameamua kutupandishia bei,” alisema Lupokela.