Home Mchanganyiko Ziara ya Kamishna Mkuu wa TRA katika kiwanda cha TBL Mbeya kukagua  uzalishaji...

Ziara ya Kamishna Mkuu wa TRA katika kiwanda cha TBL Mbeya kukagua  uzalishaji wa ETS

0

Kamishna Mkuu wa TRA, Dk.Edwin Mhede (katikati)  na ujumbe wake wakipata maelezo ya matumizi ya mfumo wa stampu za Kieletroniki unavyofanya kazi kutoka kwa Meneja wa ETS, wa kiwanda hicho, Ibrahimu Marwa,walipofanya ziara ya kikazi katika Kiwanda cha TBL cha Mbeya.

Ujumbe wa Kamishna Mkuu wa TRA ukitembezwa katika vitengo mbalimbali vya uzalishaji wa Bia katika Kiwanda cha TBL cha Mbeya.

******************************

 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Dk.Edwin Mhede, wiki iliyopita alifanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Mbeya, ambapo alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha TBL na kujionea jinsi kinavyofanya uzalishaji wa bia kwa kutumia mfumo wa Serikali wa  Stampu za kodi za kielekitroniki (ETS).

Meneja wa kiwanda hicho,Godwin Fabian,alimweleza Kamishna Mhede na ujumbe wake kuwa TBL chini ya kampuni mama ya ABInBEV, inatumia mfumo wa ETS katika viwanda vyake vyote na inaamnini kuwa inasaidia kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki kwenye masoko mbali na kuongeza mapato ya Serikali.

TBL Group. ni moja ya kampuni kinara inayoongoza kwa kulipa na kukusanya kodi za Serikali ambapo imefanikiwa kutunukiwa tuzo ya Mlipa Kodi Bora nchini sambamba na tuzo ya Rais ya  Mzalishaji bora.