Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine akizungmza na wahitimu wa kidato cha nne wapatao 263 yaliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita.
Baadhi ya Wahitimu wa kidato cha nne wakituimbiza wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzoa katika mahafali yao yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Shantamine.
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti mwanafunzi bora, Editha Karlo aliyekuwa akiongoza masomo kwa jumla ya Wahitimu 263 wa kidato cha nne wakati wa mahafali yaliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita.
Diwani wa kata ya Mtakuja, Constantine Morandi akizungumza na wahitimu wa kidato cha nne kabla ya Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wapatao 263.
************************
NA MWANDISHI WETU- GEITA
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa chakula katika shule ya Sekondari ya Shantamine.
Amesema ataitoa fedha hiyo kwa ajili ya kupunguza adha kwa wanafunzi wa shule hiyo wanaolazimika kukaa nje wakati wa kula chakula hasa katika kipindi cha mvua.
Ahadi hiyo ameitoa leo mkoani Geita wakati alipokuwa akizungumza na jumla ya Wahitimu 263 wa kidato cha nne kwenye mahafali yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Shantamine.
Ombi hilo linakuja kufuatia risala iliyosomwa kwake na Wahitimu wa kidato cha nne wakiomba kukamilishiwa ujenzi wa ukumbi huo utakaoweza kuwahudumia wanafunzi wengi kutokana na idadi yao kuongezeka hali inayowalazimu kupata shida wakati mvua ikiwa inanyesha
Katika hatua nyingine, Mhe. Kanyasu ameahidi kuchimba kisima kirefu zaidi katika shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kike wanaolazimika kutoka nje ya shule kutafuta maji
Ameeleza kuwa maombi kwa ajili ya uchimbaji wa kisima hicho yamewashawasilishwa katika wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wanachosubili ni utaratibu wa namna ya kukichimba kisima hicho.
Hata hivyo Mhe. Kanyasu ameeleza kuwa jumla ya visima viwili vilishachimbwa katika shule hiyo lakini ilibainika kuwa havina maji na eneo hilo lilionekana kuwa maji yake yana chumvi sana.
Akizungumzia kuhusu ombi la kupatiwa umeme katika shule hiyo, Mhe. Kanyasu amesema ifikapo mwezi mei mwakani shule hiyo itakuwa tayari ina umeme.
Aidha, Mhe. Kanyasu amewaahidi wanafunzi wa shule hiyo kuwa atashirikiana na madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita kujenga mabweni kadiri pesa inavyojitokeza ili kuwanusuru wanafunzi wanaolazimika kupanga nyumba nje ya shule hali inayopelekea wanafunzi wengi wa kike kuacha masomo baada ya kupata mimba.
Mbali na hilo, Mhe. Kanyasu amewatakia heri wahitimu hao katika mitihani yao na kuwataka wasiridhikena elimu hiyo na badala yake wajiendeleze zaidi
Naye. Diwani wa Kata ya Mtakuja. Constantine Morandi amewataka wananfunzi hao wajiandae kikamilifu katika mitihani ya kuhitimukidato cha nne ili kuweza kuileta sifa shule hiyo
‘’Nina washukuru wazazi pamoja na waalimu kwa ushirikiano wenu katika kuhakikisha wanafunzi 263 wanahitimu masomo yao’
Akizungumza mhitimu wa kidato cha nne kwa niaba ya wenzake , Anna Masumbuko amesema wapo tayari kwa ajili ya mtihani wa mwisho na wanategemea kufaulu vizuri katika mitihani yao.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Kikula Swillah amesema wanafunzi hao wamejianda vema na shule inategemea wanafunzi watafaulu na kujiunga na kidato cha tano na wengine waliobaki watachaguliwa katika vyuo vya ufundi