Home Michezo KIPCHONGE AWEKA REKODI YA DUNIA MBIO ZA MARATHON

KIPCHONGE AWEKA REKODI YA DUNIA MBIO ZA MARATHON

0

****************************

EMMANUEL MBATILO

Mwanariadha kutoka nchini Kenya Eliud Kipchoge amekuwa mwanariadha wa kwanza duniani kutumia chini ya saa 2 kumaliza mbio za marathon (Kilomita 42).

Mwanariadha huyo ametimiza ndoto yake na kuweka rekodi mpya ya dunia leo nchini Austria akitumia saa 1, dakika 59 na sekunde 40.2 (1:59:40.2) kwenye mashindano maalum ya INEOS 1:59 Challenge.

Kipchoge amevunja rekodi yake binafsi ya kutumia saa 2:01::39 aliyoiweka mwaka jana kwenye Marathon ya Berlin.