Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Viongozi wa Mkoa wa Katavi, Mawaziri pamoja na Wabunge akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa umeme wa kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa kwa njia ya msongo wa Kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora katika sherehe fupi zilizofanyika nje kidogo ya manispaa ya Mpanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani mara baada ya kuweka la msingi mradi wa umeme wa kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa kwa njia ya msongo wa Kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora katika sherehe fupi zilizofanyika nje kidogo ya manispaa ya Mpanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuweka la msingi mradi wa umeme wa kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa kwa njia ya msongo wa Kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora katika sherehe fupi zilizofanyika nje kidogo ya manispaa ya Mpanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi na wafanyakazi wa Tanesco mara baada ya kuweka la msingi mradi wa umeme wa kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa kwa njia ya msongo wa Kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora katika sherehe fupi zilizofanyika nje kidogo ya manispaa ya Mpanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanafunzi wa Isukumilo na Mpanda Sekondari wakati akielekea Wilaya Mpya ya Tanganyika.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Isukumilo na Mpanda Girls wakimsangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama katika barabara ya kuelekea katika Wilaya mpya ya Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ramani ya majengo ya hospitali ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wakati akipewa maelezo na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo katika eneo la mradi huo wa ujenzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine wa mkoa wa Katavi, Wabunge pamoja na Mawaziri, akivuta utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Hospitali za Wilaya ya Tanganyika, Mlele na Mpimbwe mkoani Katavi mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo mpya ya Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando mara baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mpanda-Ifukutwa-Vikonge km 35 katika eneo la majalila Wilayani Tanganyika mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke wake Mama Janeth Magufuli, Mawaziri, viongozi wa mkoa wa Katavi pamoja na Wabunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Mpanda-Ifukutwa-Vikonge km 35 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la majalila Wilayani Tanganyika mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera mara baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya Mpanda-Ifukutwa-Vikonge km 35 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la majalila Wilayani Tanganyika mkoani Katavi. PICHA NA IKULU