Na Mwandishi Wetu, CAIRO
YANGA SC itamenyana na Pyramids ya Misri katika mechi mbili za nyumbani na ugenini kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Hiyo ni baada ya droo iliyopangwa leo mjini Cairo mjini Misri na wawakilishi hao wa Tanzania wakifanikiwa kuvuka hatua hiyo wataingia kwenye makundi.
Yanga imeangukia katika mchujo baada ya kutolewa na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia sare ya 1-1 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-1 Ndola.
Katika Raundi ya kwanza, Yanga iliitoa Township Rollers ya Botswana kwa mabao 2-1, ikishinda 1-0 Gaborone baada ya sare ya 1-1 Dar es Salaam. Hii ni mara ya tano Yanga SC inafika hatua hii, mara zote ikiporomoka kutoka kwenye Ligi ya Mabingwa na mara mbili tu ilifanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shrikisho.
Mwaka 2007 ilitolewa na El-Merreikh ya Sudan baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kabla ya kwenda kuchapwa 2-0 Khartoum, kufuatia kutolewa na Esperance ya Tunisia katika Ligi ya Mabingwa.

Mwaka 2017 ilitolewa na MC Alger ya Algeria baada ya kufungwa 4-0 Algiers kufuatia kushinda 1-0 Dar es Salaam ikitoka kutolewa na Al-Ahly ya Misri baada ya kufungwa 2-1 Alexandria kufuatia sare ya 1-1 Dar es Salaam.
Mwaka 2016 ilifuzu kwa mara ya kwanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kuitoa Sagrada Esperança kwa ushindi wa 2-0 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 1-0 Angola ikitoka kutolewa na na Zanaco ya Zambia kwa bao la ugenini baada ya sare ya 1-1 nyumbani na 0-0 ugenini.
Mwaka 2018 ilishiriki tena hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kuitoa Welayta Dicha ya Ethiopia kufuatia ushindi wa 2-0 Dar es Salaam kabla ya kwenda kupigwa 1-0 Ethiopia ikitoka kutolewa na Township Rollers ya Botswana kwa kufungwa 2-1 Gaborone kufuatia sare ya 0-0 Dar es Salaam