Home Mchanganyiko MKOPO WA ZAIDI YA TSH. BILIONI 78 YAWANUFAISHA WANAWAKE, VIJANA NA WATU...

MKOPO WA ZAIDI YA TSH. BILIONI 78 YAWANUFAISHA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KAGERA

0
Na Silvia MChuruza,Karagwe.
Mkuu wa mkoa kagera Brigedia  General Marko Gaguti amekabidhi zaidi ya Tsh. Bilioni 78 ikiwa ni mkopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wilayani karagwe.
Akizungumza na wanavikundi hao Mhe.Gaguti ,amesema kuwa serikali itahakikisha mikopo hiyo haitozwi riba ikiwa ni agizo kutoka kwa Raisi wa awamu ya tano kuhakikisha wanawake,  vijana na watu wenye ulemavu wanapata mikopo ili  kujikwamua kiuchumi.
Hata hivyo Gaguti amepongeza juhudi za uongozi wa wilaya ya karagwe kwa kusimamia mapato ya wilaya na kuto asilimia kumi kwaajili ya mikopo hiyo kwa zaidi ya vikundi 29 kwa kutimiza vigezo na kupata sifa za msingi na kuhakikisha vikundi vinatimiza malengo yaliyokubaliwa na vikundi hivyo.
Vilevile ameongeza kwa kuwataka wanavikundi kurudisha mikopo hiyo kwa wakati kutokana na mikopo hiyo kutokuwa na riba.
”Hivyo Serikali itaendelea kutoa elimu ya fedha kwa vikundi hivyo ili waweze kunufaika zaidi”amesema Mhe.Gaguti
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Bi. Edina Kabyazi amesema kuwa vijana imekuwa ngumu kwao kurudisha mikopo kwa wakati sahihi, lakini pia ameongeza kuwa baada ya kuwapatia mikopo hiyo wanavikundi wanapatiwa miezi mitatu kwa ajili ya kuwasilisha changamoto zao.
Sambamba na hayo nao wanavikundi hao wameushukuru uongozi wa wilaya ya karagwe kwa kutambua umuhimu wa mikopo hiyo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuahidi kuitumia vizuri mikopo hiyo ambayao wamekabidhiwa leo.