Home Mchanganyiko KUMBILAMOTO AFANYA UKAGUZI MACHINJIO YA VINGUNGUTI

KUMBILAMOTO AFANYA UKAGUZI MACHINJIO YA VINGUNGUTI

0

Na Humphrey Shao,Jamhuri Digital
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto leo amefanya ziara katika Machinjio ya Vingunguti kukagua namna jinsi ujenzi unavyondelea na kuzungumza na wamachinga na Mama lishe namna Manispaa ilivyojipanga kuboresha  eneo la kufanyia biashra ndani ya siku saba.
akizungumza na wafanyabiashara hao Mstahiki Meya, Omary Kumbilamoto amesema kuwa manispaa imeamua kuboresha eneo la nje ya machinjio ambapo vijana na mamalishe wanafanyabiashara zao ambalo kwa sasa lipo katika mazingira mabovu.
“nimekaa na mkurugenzi wangu tkaona si vyema hapa panajengwa machinjio ya kisasa alafu hatua chache tu wenye nchi yao mnafanya biashara katika mazingira magumu hivyo tunawaomba mtupishe kwa muda wa siku saba hili tuweze kurekebisha eneo hili kwa kujenga vizimba vya mama lishe na vya kuchomea nyama pamoja na kuweka paa la juu hili tuweze kuwawekea mazingira bora ya kufanya kazi” amesema Kumbilamoto.
Pia kumbilamoto alipata fursa ya kutembelea eneo ambalo machinjio mapya yanajengwa na kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi na kusema kwa uharaka huo anaamini mafundi hao wa shirika la nyumba la Taifa watamaliza ujenzi huo ndani ya muda uliopangwa kama Mh Rais Dk. John Pombe Magufuli alivyoagiza.
aidha kumbilamoto alipata fursa ya kutembelea eneo ambalo wanataraji kuwahamishia wauza nyama inayochinjwa katika machinio hayo ya kisasa hili wasiwe mbali na eneo lao .
amesema machinjio mapya yamekuja na changamoto nyingi hivyo nasi tunakabiliana nazo kama viongozi hivyo tupo katika mazungumzo na watu wa Wizara ya Kilimo hili waweze kutupatia eneo lao lililopo jirani na machinjio hili tuweze kujenga soko la kuuzia nyama kwa muda wakati marekebishi ya soko lao yakiwa yanaendelea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na wafanyabishara waliopo nje ya machinjio ya Vingunguti ambao wanataraji kuboreshewa eneo lao la lufanyia kazi.

 Mmoja ya Mama Lishe wanaofanya biashara katika eneo hilo akimshukuru Mstahiki meya kwa hatua ya waliyofikia kuwaboreshea eneo lao la Biashara.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua eneo la Wizara ya Kilimo ambalo wauza nayama wanatakiwa kuhamishiwa kwa muda

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akivuka vidimwi vya maji kukagua eneo la wafanyabiashra ndogondogo nje ya machinjio ya Vingunguti

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza jambo na mkandarasi anayejenga Machinjio ya Vingunguti kutoka shirika la nyumba la Taifa 

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akipasua mawe katika site ya ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti