Home Michezo YANGA SC YAFUTA ‘MKOSI’ LIGI KUU VODACOM YAICHAPA 1-0 COASTAL UNION

YANGA SC YAFUTA ‘MKOSI’ LIGI KUU VODACOM YAICHAPA 1-0 COASTAL UNION

0

Timu ya Yanga hatimaye imefufuka Ligi Kuu ya Vodacom mara baada ya kupata Pointi tatu kwa kuichapa Coastal Union kutoka Tanga bao 1-0 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga imecheza mechi tatu na kujikusanyia Pointi 4 ikipoteza moja,sare moja na kushinda moja mchezo wa leo ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili.

Hadi zinakwenda mapumziko zilikuwa hazijafungana na kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko na kuwasaidia Yanga kupata ushindi.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na kiungo mkabaji kwa kichwa Abdulaziz Makame dakika ya 51 na kuwaamsha mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani.

Kwa matokeo hayo Yanga wamefikisha pointi 4 huku wakiwa wamecheza mechi tatu za Ligi kuu huku Mzunguko wa nne wanatarajia kusafiri kwenda kanda ya ziwa kucheza na Alliance pamoja na Mbao FC.