Home Mchanganyiko Mrundikano wa majukumu ya wazazi kikwazo cha elimu Njombe

Mrundikano wa majukumu ya wazazi kikwazo cha elimu Njombe

0

***************************

NJOMBE

Mrundikano wa majukumu ya majukumu,mila na destuli zilizopitwa na wakati pamoja na wazazi kuwashirikisha watoto katika masuala ya biashara wangali shuleni vimetajwa kuwa vikwazo vikuu vinavyokatisha ndoto za wanafunzi wengi mkoani Njombe.

Kukithiri kwa vikwazo hivyo ambavyo vimekua kwa kasi miaka ya hivi karibuni hususani katika maeneo ya vijijini vinamsukuma askofu wa jimbo la Njombe Padre Elasmo Mligo pamoja na mkuu wa shule ya sekondari Josephine Damas Mwalongo kutoa rai kwa jamii za mkoa wa Njombe kuvipinga kwa kuvipiga vita ili visiweze kuendelea kutekelezwa.

Ikumbukwe maeneo mengi ya vijiji yamekuwa yakiripotiwa mikasa ya wazazi kujikita katika kilimo na biashara za mazai zaidi na kupunguza uangalizi wa watoto huku wengine wakiwataka kufanya vibaya katika mitihani ili wasiweze kuendelea na masomo hatua za juu zaidi kwa lengo la kupata usaidizi katika kazi zao.

Wakati rai hiyo ikitolewa kwa jamii baadhi ya watahiniwa akiwemo Betrice Msovela na Joyce Eugen wanaelezea maandalizi na matarajio yao katika mtihani wao wa mwisho wa kidato cha nne huku pia wakitoa rai kwa wazazi ambao wanajikita zaidi kwenye kutafuta maisha na kujikuta wakisahau jukumu la malezi kwa watoto hususani wanaosoma.

Jacklin Nziku na Heronius Mswata ni wazazi ambao wameshindwa kuzuia hisia zao kwa watoto ambao wamekuwa wakitumbukia kwenye mahusiano ya kimapenzi wangali wanafunzi na kuharibu ndoto zao baada ya kupata ujauzito huku pia wakikiri mzigo wa majukumu waliyo nayo unavyo athiri malezi katika familia.

Shule ya sekondari ya wasichana ya Josephine imefanikiwa kuwatunuku vyeti wahitimu 47 wa kidato cha nne katika mahafali ya 5 tangu ianzishwe.