Home Mchanganyiko Makamu wa Rais akutana na Menejimenti ya Ofisi yake

Makamu wa Rais akutana na Menejimenti ya Ofisi yake

0

***********************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, ameitaka Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kuzingatia utendaji kazi kwa ufanisi zaidi hasa katika suala zima la kuwatendea haki wafanyabiashara walioitikia wito wa kutengeneza Mifuko Mbadala wanaoagiza  mali hafi kutoka Nje ya Nchi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo alipokutana na Menejimenti ya Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mtumba Jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumzia suala zima la Utendaji kazi Ikiwemo Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Mazingira.

Amewataka Viongozi hao kuongeza bidii ya kazi pamoja na Ushirikiano ndani ya Wizara ili kuweza kuboresha ufanisi wa utendaji kazi kwa Watumishi wa Wizara hiyo.