Home Mchanganyiko MHE. MKUCHIKA NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA...

MHE. MKUCHIKA NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA KLABU YA KUPINGA RUSHWA YA SHULE YA SEKONDARI MTANGALANGA WILAYANI NEWALA

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akishiriki kuupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika Halmashauri ya Mji Newala.

Baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Mji Newala waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru mara baada ya ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2019 kuwasili katika halmashauri hiyo ya mji na kufanikiwa kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha za Serikali.

Mwenge wa Uhuru ukiwa mbele ya Zahanati ya Tupendane iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2019 kuitembelea Halmashauri ya Mji Newala na  kukagua ujenzi wa jengo hilo ili kujiridhisha na ubora wa jengo ikiwa ni pamoja na matumizi ya fedha za Serikali zilizotolewa na Serikali kujenga zahanati hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mji Newala waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru mara baada ya ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2019 kuwasili katika halmashauri hiyo ya mji na kufanikiwa kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha za Serikali.