Home Biashara EQUITY BANK YAJA NA MUONEKANO MPYA

EQUITY BANK YAJA NA MUONEKANO MPYA

0
Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Equity, Dk. James Mwangi, akiwaonesha Logo mpya ya Benki ya Equity, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo Uganda, Apollo Makubuya (katikati) na  Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Logo hiyo iliyozinduliwa Makao Makuu ya benki hiyo Upperhill, Nairobu nchini Kenya Oktoba 2 mwaka huu. 
************************************
NAIROBI, Kenya
BENKI ya Equity imezindua muonekano mpya wa logo ya benki hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuboresha utendaji kazi wa benki hiyo katika huduma na uboreshaji wa maisha ya watu ikidhamiria kuwa benki ya mfano Barani Afrika.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Equity, Dk. James Mwangi, zilisema kuwa muonekano mpya   utaleta ufanisi katika huduma za kifedha, hasa kwenye uwanja wa utoaji wa huduma kielektroniki.
Alisema logo hiyo ni ya kipekee na imekuja wakati mwafaka katika kuleta mapinduzi kwa wateja wao, baada ya kupata ujuzi kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mjini hapa, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu, Dk. James Mwangi alisema, 
“Muonekano wetu mpya una akisi mtazamo mpya wa kibiashara, wateja na kuleta matokeo bora kwenye benki kuelekea katika mafanikio ya baadae pasipo na kusahau tulikoanzia”.
Alisema Benki ya Equity imedhamiria kuwa na ubora wake kwa kuzingatia malengo na dhamira ya kuwahudumia wateja kwa kuwawezesha  wafanyabiashara na wajasiriamali kupitia huduma zenye ubunifu na za kisasa. Uimarishaji wa huduma za kielektroniki pia utasawadia wateja wa Equity Bank kufungua fursa mpya za kibenki katika mfumo wa kielektroniki kwa kuangazia kuleta ufanisi katika ugunduzi wa huduma zake za kibiashara.
Equity Bank iliyoanza kutoa huduma miaka 35 iliopita na hadi sasa inatoa huduma za kimkakati katika nchi 9 za Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, South Sudan, Rwanda, Democratic Republic of Congo (DRC),  Zambia, Msumbiji na Ethiopia.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Makampuni ya Equity, Mhandisi. Raymond Mbilinyi (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti (katikati) na Mkurugenzi asiyekuwa na majukumu, Dino Stengel wakifurahia jambo wakati wakipiga picha ya pamoja mbele ya bango lenye Kogo mpya ya Benki hiyo ya Equity wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Oktoba 2, mwaka huu Makao Makuu ya benki hiyo, Upperhill, Nairobu nchini Kenya.