MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambapo kiwilaya ilifanyika kwenye ukumbi wa Halamshauri ya Korogwe mji wilayani Korogwe kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika la African Women Aids Working Group (AFRIWAG) mkoani Tanga Magreth Ruhinda
|
Mwenyekiti wa Shirika la African Women Aids Working Group (AFRIWAG) mkoani Tanga Magreth Ruhinda akitoa taarifa yao wakati wa maadhimisho hayo |
|
Mwakilishi wa Shirika la Help Age Internation Martha Kihampa akizungumza wakati wa maadhimisho hayo |
|
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo |
|
Sehemu ya wazee kutoka maeneo mbalimbali wilayani Korogwe wakiwa kwenye maadhimisho hayo |
Sehemu ya wazee wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akilakiwa na Mwenyekiti wa Shirika la African Women Aids Working Group (AFRIWAG) mkoani Tanga Magreth Ruhinda
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kulia akiagana na Mwakilishi wa Shirika la Help Age Internation Martha Kihampa mara baada ya kufungua maadhimisho hayo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua maadhimisho hayo
*****************************************
MKUU wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Kissa Gwakisa ametaka wazee kuendelea kupewa elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa ukimwi ili kuweza kuepukana nayo ambayo ni hatari kwa ustawi wa jamii pindi wanapokumbana nayo.
Kissa aliyasema hayo wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambapo kiwilaya ilianzimishwa kwenye ukumbi wa Mji wa Korogwe ambapo alisema wazee ni kama binadamu wengine hivyo lazima wapatiwe elimu hiyo ili waweze kuchukua tahadhari.
Alisema kwani wanapokuwa wakijitibu magonjwa ya namna hiyo wakiwa na umri mkubwa ni gharama na ngumu sana kwao huku akiwataka waendelee na mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
“Ndugu zangu wazee lazima tutambue kwamba kuna ugonjwa hatari wa ukimwi hivyo upo uhimu wa kuendelea kupatiwa elimu kuhusiana na ugonjwa huo kwani ni wanapojitibu ugonjwa huo mkiwa na umri mkubwa ni gharama kubwa sana “Alisema.
Aidha alisema kwamba kwenye maeneo yanatotoa huduma wananchi watambua ni jukumu lao la kutunza wazee huku akieleza kwamba serikali iliagiza wazee wanapokwenda hospitalini watibiwe kwa haraka na dawa wazipate kwa wakati.
“Watumishi wa afya hakikisheni wazee wanahudumiwa vizuri mtu ambaye hataki kumuhudimua mzee vizuri kwa sababu ni mzee atoke kwenye hispitali zaserikali aende akatafute kazi nyengine ya kufanya”Alisema.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba watanzania wamelelewa kuheshimu wazee kwani hakuna mtu ambaye hatafika kwenye uzee hivyo serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuweza kuondosha changamoto zinazowakabili.
Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Shirika la African Women Aids Working Group (AFRIWAG) mkoani Tanga Magreth Ruhinda alieleza vikwazo ambazo vimekuwa vikiwakabili wazee nchini na kujikuta wakishindwa kufikia malengo yao ambavyo vimegawanyika kwenye makundi manne.
Magreth alibainisha vikwazo hivyo vinatokana na unyanyasaji wa ukiukwaji wa haki za wazee,umaskini wa kipato,huduma duni za afya na matibabu ikiwemo zinazotokana na ugonjwa hatari wa Ukimwi.
Aidha alisema kutokana na uwepo wa changamoto hizo shirika hilo kwa kushirikiana na wenzao wa Kimataifa wa Help Age wamefanikiwa kutekeleza mradi wa kuboresha afya za wazee kwenye halamshauri ya wilaya ya mji wa Korogwe .
Mwenyekiti huyo alisema kwamba utekelezaji huo unafanyika chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza na kisiwa cha Jersey ambao umewezesh mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa baraza Halmashauri na Mabaraza ya kata.
Alisema pia wataendelea kutoa mafunzo kwa watumishi 33 katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuongeza uelewa kwa watumishi kuhusu namna ya kutoa huduma rafiki za afya kwa wazee, magonjwa yasiyoambukizwa, kutambua hali za uzee zinazowakabili na afya ya uzazi.
Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Wazee kutoka Baraza la Halmashauri ya Korogwe mji Mtafi Hassani alisema kwamba kundi hilo linakabiliwa na chanagmoto mbalimbali ambazo hazina budi kupatiwa ufumbuzi na serikali kuu na serikali za mitaa ikiwemo za kiafya,kiuchumi na sauti zao kutokusikilizwa mara kwa mara huku akieleza kwamba wanahitaji kusikilizwa kwa jicho la kipekee kwa dhati na vitendo.
“Tunaiomba serikali ya Rais Dkt John Magufuli isikie kilio chetu kama ilivyo kwa makundi mengine …Lakini sera ya wazee ya mwaka 2003 ambayo imesheheni matamko mengi ya kisera yanayodhihirisha utashi wa kisiasa wa serikali yetu hadi sasa haijatungiwa sheria toka iliopopitishwa mwaka 2003 hivyo tunaomba serikali ya awamu hii ya tano iharakishe mchakato wa kutungiwa sheria iweze kutekelezeka”Alisema
Mtafi ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wazee Mtaa wa Mtonga Kata ya Mtonga wilayani humo aliipongeza serikali kwa kutoa msamaha wa matibabu kwa wazee kila wanapokwenda kutibiwa katika hospitali za serikali na umma ikiwemo kuongeza dawa na watumishi katika vituo vya kutolea huduma ikiwemo kuboresha miundombinu ya vituo hivyo.