Home Mchanganyiko Rais Dkt.Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamuhuri ya Watu wa...

Rais Dkt.Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China Xi Jinping

0

**********************

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi
Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China Xi Jinping pamoja na
wananchi wa Taifa hilo kwa kuadhimisha miaka 70 tangu
kuundwa kwake.

Katika salamu zake alizotuma kwa Rais Xi Jinping, Dk.
Shein amesema kwa niaba ya wananchi na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar anatoa pongezi za dhati kwa Taifa
hilo kwa mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii
yaliofikiwa, katika kipindi hicho.

Amesema Zanzibar inajivunia urafiki na uhusiano mzuri
wa kihistoria uliopo kati yake na Serikali ya Jamuhuri ya
Watu wa China, ikiwa ni matokeo yatokanayo na uongozi
bora na uliotukuka kutoka kwa mwasisi wa Taifa hilo
Mwenyekiti Mao Zedong.

Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inaunga mkono juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Taifa hilo , ikiwa ni hatua ya kuunga mkono mawazo ya muasisi wake Mweyekiti Mao.

Rais Dk. Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itaendeleza uhusiano wa kindugu na ushirikano
uliopo kati yake na Jamuhuri ya Watu wa China, kwa
maslahi ya wananchi wake.

Aidha, Dk. Shein ametumia fursa hiyo kumtakia afya
njema na maisha yenye furaha Rais Xi Jinping pamoja na
wananchi wote wa Taifa hilo.