Meneja wa Tanesco Wilaya ya Gairo Bw. Isack Emmanuel Mwaipopo akiongea na wananchi wa kata ya idibo wilayani gairo  wakati wa ziara ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya vishoka na utunzaji wa miundombinu ya umeme katika wilaya hiyo.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Idibo wakiwasikiliza maofisa kutoka Tanesco (hawapo pichani) ambao wnawapatia elimu juu ya vishoka.

………………………………………

Na farida Saidy, Morogoro

Katika kuhakikisha wananchi wanaepukana na matapeli wanaounganisha umeme manyumbani ambao hawajasajiliwa maarufu kama  VISHOKA Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Morogoro linaendelea kutoa elimu kwa wanachi hususani wanaopitiwa na mradi wa REA.

Akizunguza na wananchi wa kata ya Idibo Wilayani Gairo Mkoani Morogoro wakati akitoa elimu jua ya kuepukana na vishoka Afisa uhusiano huduma kwa wateja Mkoa wa Morogoro  Jacqueline Lusozi amewataka wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme wawasiliane na ofisi ya tanesco wilaya ili waweze kupata maelekezo yaliosahihi pamoja na kupata mafundi wenyevigezo.

Hata hivyo amewataka wananchi waliofikiwa na mradi wa REA awamu wa tatu mzungumko wa kwanza kwa Wilayani Gairo  wanaotaka kuchukua fomu za tanesco kwa ajiri ya kuunganishiwa umeme huo wanatakiwa kuwa na kitamburisho cha kupigia kura,reseni ya gari au pikipiki na kitamburisho cha nida.

kwa upande wake meneja wa tanesco Wilaya ya Gairo Bwana Isack Emmanuel Mwaipopo amewatoa hofu wananchi wa kata ya idibo kuwa watapata umeme kabla ya mwezi disemba, kwani  mkandalasi bado anaendelea na kazi hivyo wawe na amani watapata umeme.

Katika hatua nyingine Bwana Mwaipopo amewataka wananchi  kuilinda na kuitunza miundombinu ya umeme itakayopita katika meneo yao sambamba na kuacha kufanya shughuri za kibinaadamu katika miundombinu hiyo ili kuepuka tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara 

Nae diwani wa kata ya idibo Bwana Rajabu Abdarah Mguhi imelishukuru shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Morogoro kwa kutoa elimu kwa wananchi wake ambayo itawasaidia kuepukana na vishoka hali itakayowasaidia kupata huduma iliyo bora na kwa wakati.

Hata hivyo Pamoja na elimu hiyo kutolewa juu ya kuepukana na vishoka tayari Baadhi ya wananchi wa kata ya idibo wameshakumbana  na vishoka hivyo wameahidi kufuata taratibu zilowekwa na shirika la umeme Tanzania.

Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Morogoro linaendea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambapo kwasasa linatoa elimu katika Wilaya ya Gairo na Mvomero.