Home Biashara CRDB Bank yazindua kampeni ya “Ulipo-Tupo”

CRDB Bank yazindua kampeni ya “Ulipo-Tupo”

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB. Abdulmajid Nsekela akiongea katika uzinduzi wa kampeni ya “Ulipo Tupo” ambayo ina lengo la kendelea kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla juu ya huduma zitolewazo na Benki ya CRDB ambazo zinamlenga mtanzania mmoja mmoja.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko. Joseline Kamuhanda akiongea katika uzinduzi wa kampeni ya “Ulipo Tupo” ambayo ina lengo la kendelea kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla juu ya huduma zitolewazo na Benki ya CRDB ambazo zinamlenga mtanzania mmoja mmoja.

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, akiongea katika uzinduzi wa kampeni ya “Ulipo Tupo” ambayo ina lengo la kendelea kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla juu ya huduma zitolewazo na Benki ya CRDB ambazo zinamlenga mtanzania mmoja mmoja.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakati. Boma Raballa akiongea katika uzinduzi wa kampeni ya “Ulipo Tupo” ambayo ina lengo la kendelea kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla juu ya huduma zitolewazo na Benki ya CRDB ambazo zinamlenga mtanzania mmoja mmoja.

Wateja na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya  uzinduzi wa kampeni ya “Ulipo Tupo” ambayo ina lengo la kendelea kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla juu ya huduma zitolewazo na Benki ya CRDB ambazo zinamlenga mtanzania mmoja mmoja.

********************************

Dar Es Salaam Tanzania, Septemba 26, 2019 – Benki ya CRDB yazindua kampeni ya Ulipo Tupo ambayo ina lengo la kendelea kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla juu ya huduma zitolewazo na Benki ya CRDB ambazo zinamlenga mtanzania mmoja mmoja.

Benki ya CRDB imekuwa kinara sokoni kwa kuongoza nchini kwa mambo yafuatayo;
 Rasilimali za shilingi trilioni 6038 ambayo ni asilimia 20.3% ya soko na hivyo
kuifanya benki kuwa kinara katika soko.

 Amana za shilingi 4.9 trilioni ambayo ni 23.3% ya soko nchini.
 Mikopo yenye thamani ya shilingi trilioni 3.18 inayoongoza kwenye soko.
 Matawi 266 na mashine za kutolea fedha (ATM) 553 na mawakala (CRDB
Wakala) 10,000.

Benki ya CRDB pia imeendelea kuwa kinara katika kusaidia maendeleo nchini kwa
kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo;
 Rufiji Hydropower Project
 Standard Gauge Railway Line
 Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Dar es Salaam
 Ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa kimataifa Dar es Salaam (Terminal 3)
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni hii, Afisa wa
Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema “Kwa muda mrefu sasa,

Benki ya CRDB imekuwa ikitumia kauli mbiu yake ya Ulipo Tupo ikibeba ahadi kwa
wateja wetu kuwa sisi kama Benki Tupo na tunaendelea kuwepo popote pale wateja watu walipo ili kufanikisha malengo tuliojiwekea” leo hii tunazidua rasmi kampeni ya “Ulipo-Tupo” tukirejea tena ahadi hii kwa wateja wetu. Ahadi hii ya “Ulipo-Tupo” tumeigawa katika makundi matatu muhimu na nitaelezea kundi moja moja..Alisema.

1. Ahadi ya kwanza ni “Savings” kujiwekea akiba.
Benki ya CRDB inaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza watanzania kuhusu njia
mbadala za kujiwekea akiba ambazo zinatolewa na Benki ya CRDB. Alisema DKT.
Joseph Witts “Benki ina bidhaa mbalimbali ambazo zitaweza kusaidia wateja na
watanzania kwa ujumla kutimiza malengo na mahitaji yao kwa kujiwekea akiba kwa ajili
ya baadae. Bidhaa hizi ni kama;
 Akaunti ya watoto (Junior Jumbo)
 Akaunti ya Vijana (Teens Account)
 Akaunti za wanafunzi (Scholar Account)
 Akaunti za mishahara (Salary Account)
 Akaunti kwa ajili ya akina mama (Malkia Account)
 Retirees Account kwa wastaafu
 Current account kwa wafanya biashara

2. Ahadi ya pili ni “Borrowing” huduma za mikopo.
Alisema Dkt. Witts kuwa “Benki imejikita katika kutoa mikopo mbali mbali kwa vikndi
mbali mbali kwa riba nafuu na kwa haraka zaidi kwa kupunguza masharti yake ili
kumuwezesha kima mtanzania kuweza kukopa na kufikia malengo yake aliyojiwekea.”
Benki ya CRDB inatoa mikopo ifuatayo;
 Mikopo binafsi “Personal Loan” kwa riba ya asilimia 16%, nafuu kabisa sokoni.
 Mikopo ya biashara
 Mikopo ya wajasiriamali
 Mikopo ua ujenzi na ununuzi wa nyumba “Mortgage”
 Mikopo ya kilimo iliyo nafuu sokoni

3. Ahadi ya tatu ni “Transanct” Urahisi wa kupata uduma za Benki
Benki imejikita kutanua mtandao wake ili kuwafikia watanzania wote na kutoa huduma
bora za kibenki kupitia;
 Matawi 266 nchi nzima

 Matawi 15 yanayotembea
 ATM 553 nchi nzima
 Wakala elfu kumi (10,000)
 Huduma ya Simbanking
 Huduma za kadi za kimataifa (Visa cards, Master cards, China union pay)
 Huduma za mtandao (internet banking)
 Mashine za POS 3,000
Afisa Biashara Mkuu wa Benki, Dkt. Joseph Witts alisisitiza tena kwa kusema “ Lengo la Benki ya CRDB ni kuhakikisha tunakuwa sehemu ya mafanikio ya maisha ya wateja wetu na watanzania kwa ujumla. Tunaendelea kukuza mtandao wetu na kueneza nchi nzima ili kuwafikia hata wale ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki na pia tuna mikakati mbadala ya kuboresha huduma zetu kupitia mifumo ya kidijitali, tukiishi kwa kauli yetu hai ya “Uli-Tupo”