Home Mchanganyiko SERIKALI NA UNICEF KUANZISHA MAFUNZO MAALUMU YA UFUNDI STANDI KWA VIJANA

SERIKALI NA UNICEF KUANZISHA MAFUNZO MAALUMU YA UFUNDI STANDI KWA VIJANA

0

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima, akizungumza wakati wa kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu alipokuwa  akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga

Sehemu ya wadau wakifatilia kwa umakini Hotuba ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima,wakati wa kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu alipokuwa  akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga jijini Dodoma.

 

 Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima,akisisitiza jambo wakati wa kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu alipokuwa  akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga jijini Dodoma.

Wadau wakimsikiliza kwa umakini Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu alipokuwa  akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga jijini Dodoma.

Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro Bi.Paulina Mbena akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima,baada ya kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu alipokuwa  akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe,akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungwa kwa  mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu uliofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.

PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG

……………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani(UNICEF) wamejipanga kuanzisha mafunzo maalumu kuwapa ujuzi na kuwakomboa vijana walio nje ya mfumo wa elimu ili nao wanufaike na mpango wa kupata stadi maisha za kuweza kujiajiri.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima, alipokuwa akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, wakati wa kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu.

Amesema wamejipanga kuhakikisha wanaanzisha mafunzo hayo kupitia IPOSA, mafunzo hayo ambayo yatawawezesha vijana walio nje ya mfumo wa elimu kupata mafunzo ya stadi za maisha na kupata ujuzi na kujiajili na kukuza sekta ya viwanda vidogovidogo.

“Sisi kama serikali kwa kushirikana na wenzetu wa UNCEF kupitia kwa IPOSA, tunawapa mafunzo vijana walio nje ya mfumo, ambao hawakuweza kupata elimu na mafunzo hayo yatawawezesha kupata stadi za maisha” amesema Dkt Dorothy.

Mbali na hapo ameshauli elimu ya ufundi ianzie kwenye elimu ya awali na  msingi ili kuwawezesha watoto kukua wakijua namna ya kuunda kitu na kujenga dhana ya stadi za maisha.

“Elimu ya ufundi inatakiwa kuanzia kwa watoto katika shule za awali na msingi ili watoto hawa wanapokuwa wanakuwa na ujuzi na wanakuwa na uwezo wa kuunda kitu au dhana ya kitu, tofauti na sasa elimu hiyo inatolewa kwa watu wazima tunakuwa tumechelewa” amesema.

Aidha amesema kama tunataka kutoka hapa tulipo na kufikia malengo ya nchi ya ifikapo 2025 tufikie uchumi wa Kati, ni lazima tushikilie elimu kwani ndio Jeshi na msingi wa hayo yote.

Amesema wao kama serikali wanajitahidi kuhusianisha kati ya elimu na Jamii ili elimu hiyo iwasaidie katika kujikwamua kupitia nyanja mbalimbali katika kutoka hapo walipo na kwenda sehemu nyingine kiuchumi kupitia elimu hiyo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe, amesema mkutano Kama huo hufanyika kila mwaka na kuna fedha ambayo hutengwa na Serikali, na washirika wengine wa maendeleo na katika mikutano kama hii hutumika kufanya tathmini ya kupitia maazimio waliojiwekea.

Pamoja na kuona utekelezaji wa maazimio hayo na kushirikisha changamoto zilizopo katika kutekeleza maazimio waliojiwekea katika kuhakikisha wana toa elimu iliyobora hapa nchini.

Pia wamekuwa na mijadala mbalimbali na katika mijadala hiyo, pia wadau wameibua suala la kuhakikisha katika mipango ya ujenzi wa vyuo na turudi katika falsafa ya kwamba Kama chuo kimeanzishwa kwa ajiri na Uvuvi kweli kijikite katika Uvuvi na kuleta tija katika sekta hiyo ya uvuvi.