Wataalam wa Tume ya Madini wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kutoa huduma kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 24 Septemba, 2019
Mtaalam kutoka Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Erick Ketagory (kushoto) akielezea majukumu ya TEITI kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 24 Septemba, 2019.
Mwananchi wa Geita, Yustian Mulaki (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST), Priscus Kaspana katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 24 Septemba, 2019.
Mtaalam kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Cleophas Siame (kushoto) akimwelekeza mmoja wa watembeleaji wa banda hilo namna ya kuangalia ubora wa madini kwa kutumia darubini katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 24 Septemba, 2019.
Wataalam kutoka Tume ya Madini, Msafiri Kussa na Asimwe Kafrika wakitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyankumbu iliyopo mkoani Geita, waliotembelea banda katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 24 Septemba, 2019
Mtaalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST), Priscus Kaspana (kulia) akitoa elimu ya madini kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyankumbu iliyopo mkoani Geita, waliotembelea banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 24 Septemba, 2019