Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria PROF. Sifuni Mchome akizungumza katika kikao na wadau mbalimbali kutoka Serikalini (hawako pichani) kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (ASIA-AFRICAN LEGAL CONSULTATIVE ORGANISATION (AALCO) utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 25, Oktoba jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria PROF. Sifuni Mchome katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali kutoka Serikalini baada ya kumalizika kwa kikao cha kufahamishana kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa AALCO utakaofanyika mwezi Oktoba jijini Dar es Salaam.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa AALCO utakaofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa AALCO utakaofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
…………………
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (ASIA-AFRICAN LEGAL CONSULTATIVE ORGANISATION (AALCO) utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 25, Oktoba jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria PROF. Sifuni Mchome amesema mkutano huo utawakutanisha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu kutoka nchi za Afrika na Asia ambao kwa pamoja wataangalia maendeleo ya sekta ya sharia na kujadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi wanachama na jinsi ya kukabiliana nazo.
Prof.Mchome amesema katika mkutano huo Tanzania itakabidhiwa kiti cha Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye atatumikia kiti hicho kwa mwaka mmoja.
Prof. Mchome alikuwa akizungumza na wadau mbalimbali kutoka Serikalini Ofisini kwake katika Mji wa Serikali Mtumba jijijini Dodoma ambao aliwaomba kuuungana na Wizara ya Katiba na Sheria katika kuhakikisha Mkutano huo utakaoitangaza nchi kimataifa unafanikiwa.
AALCO ilianzishwa mwaka 1956 kwa lengo la kuwa chombo cha ushauri na ushirikiano katika masuala ya sheria za kimataifa kwa nchi za Asia na Afrika.
Toka kuanzishwa kwake AALCO imewezesha nchi wanachama kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya sheria za kimataifa na kimechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria za kimataifa.
Tanzania ilijiungana umoja huo 1973 na kwa sasa Katibu Mkuu wake ni Mtanzania Prof. Gastorn ambaye alichaguliwa kushika nafasi hiyo mwezi Agosti 2016.