Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika mahafali ya 14 ya shule ya Kibaha Indepent Lisa Vicent kushoto kwake ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shule hiyo Alhaji Yusuph Mfinanga akifuatiwa na Mkuu wa shule hiyo Charles Majani.
Baadhi ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika shule ya msingi ya Kibaha Independent wakionyesha umahiri wao wa kuimba na kucheza wimbo maalumu ambao uliandaliwa kwa ajili ya mahafali ya 14 ya shule hiyo kwa ajili ya kuwaaga
Wanafunzi waliomaliza darasa la saba katika shule ya msingi Kibaha Kibaha Independent wakicheza kwa furaha katika sherehe ya mahafali yao ya 14 ambayo ilihudhuliwa na viongozi mbali mabli wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
PICHA NA VICTOR MASANGU
………………….
VICTOR MASANGU, PWANI
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amechukizwa na kukemea vitendo vya uvunjifu wa amani ambavyo vinavyofanywa na baadhi ya makundi ya watu ambao ni waharifu kuamua kuwateka watoto wa shule ambao hawana hatia na kuwaonya kuachana mara moja na tabia hiyo na kuwataka wazazi na walezi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuwafichua ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe ya mahafali ya 14 ya darasa la saba katika shule ya msingi Kibaha Independent ambapo pia amewaasa wanafunzi wote waliohitimu kutojiingiza kabisa katika makundi ya uvutaji wa madawa ya kulevya,mahusino ya kimapenzi,uhalifu na badala yake wahakikishe wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuzingatia elimu ambayo wameipata kwa lengo la kutimiza malengo waliyojiwekea.
“Kwa kweli ndugu wazazi na walezi kwa sasa kumeanza kuingia kwa baadhi ya watu kuwateka watoto wetu wa shule na hivi karibuni kumetokea mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari Tumbi kutekwa na watu wasijulikana katika mazingira ya kutatanisha na kumpakia kwenye gari ndogo kisha kwenda kumtelekeza maeneo ya ubungo jijini Dar es Salaam, kwa hiyo kwa sasa bado tunaendelea na msako kwa ajili ya kuwatafuta wahusika,”alisema Ndikilo.
Aidha Ndikilo katika hatua nyingine aliupongeza uongozi wa shule ya Kibaha Independent kwa juhudi wanazozifanya katika uboreshaji wa elimu kwa wanafunzi wao ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba katika ngazi ya taifa na kuwataka walimu waendelee na bidii zaidi ili waweze kushika nafasi ya kwanza katika mitihani yao waliyoimaliza hivi karibuni.
“Walimu wa Kibaha Indep[endent kwa kushirikiana na bodi yote ya wakurugenzi kwa kweli mnafanya kazi nzuri na serikali ya awamu ya tano itaendelea kushirikiana bega kwa began a shule binafsi lengo ikiwa ni kuhakikisha watoto wetu wote wanapata elimu ambayo itawasaidia katika siku za baadae katika kuliletea Tiafa maendeleo kutokana na mahalifa ambayo wameyapata katika sekta ya elimu,”alisema Ndikilo.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Kibaha Independent Charles Majani amempongeza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuboresh sekta ya elimu na kuiomba serikali kuwasaidia upatikanaji wa vibali kwa wakati kwa ajili ya kuanzisha shule mpya nyingine ambayo itaweza kutoa fursa zaidi ya kutoa taaluma kwa wanafunzi bila ya kuwa na vikwazo vyovyote ambayo vinaweza kupelekea kukwamisha malengo waliyojiwekea katika suala la kutoa elimu.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shule hiyo Alhaji Yusuph Mfinanga amewataka wazazi na walezi kuwalinda kikamilifu watoto wao na kuepukana na matapeli katika suala zima la ulipaji ada,na kuwaasa watumie mfumo ambao umewekwa wa kufanya malipo kwa kutumia njia ya taasisi za kibenki ili kuondokana na usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza.
Hama mmoja wa wanafunzi akisoma rusala kwa niaba ya wahitimu wenzake alisema kuwa elimu waliyoipata imewatoa ujinga na kwamba lengo lao kubwa ni kufika mbali zaidi hadi ngazi ya vyuo vikuu na kuwashukuru walimu wao ambao wameweza kushirikiana nao bega kwa bega katika kipindi chote cha miaka saba kwa kuwapatia elimu na mahalifa katika maisha yao.
HIVI karibuni Wilayani Kibaha mkoani Pwani kulitokea tukio la kutekwa kwa mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili katika shule ya sekondari tumbi na watu wasiojulikana na kumtelekeza katika maeneo ya Ubungo Jijijni Dar es Salaam.