Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati akiongoza kikao cha mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) Mkoa wa Singida yaliyohusu kampeni shirikishi ya Surua-Rubella yaliyofanyika mjini hapa leo. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida (RAS) Dkt. Angelina Lutambi.
Dkt.Khalid Ng’ombo kutoka Mari’e Stops Tanzania akichangia jambo.
Wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia mafunzo.
Wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia mafunzo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Ernest Mugetta akizungumza kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa kamati wakichukua maelezo ya mafunzo hayo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida (RAS) Dkt.Angelina Lutambi akichangia jambo.
Mtaalamu wa Jinsia na Utetezi kutoka Shirika la World Vission Tanzania, Tumain Fred akizungumzia kuhusu watumishi kushiriki kampeni hiyo ya chanjo.
Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas akitoa mada.
Mratibu wa Huduma ya Chanjo Mkoa wa Singida, Jadil Mhanganonya akitoa mada kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Mwakilishi wa Meneja Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la USAID- Boresha Afya-EGPAF, Dkt. Nicholaus Njoka akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la Sema, Jacob Kanka akichangia jambo katika mafunzo hayo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametaka mkoa huo kutoka katika asilimia 98 ya kampeni ya chanjo ya surua rubella na polio ya mwaka 2014 kitaifa na kufikia asilimia 100 mwaka 2019.
Kauli hiyo aliitoa katika kikao cha mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya afya ya msingi (PHC) Mkoa wa Singida yaliyohusu kampeni shirikishi ya Surua- Rubella na polio yaliyofanyika mkoani hapa jana.
Alisema suala hilo la chanjo si la mchezo ni la kitaaluma halitakiwi kuathiriwa hivyo wao kama mkoa waikatae asilimia hiyo ya 98 na kufikia asilimia 100.
“Sisi katika chanjo ya kitaifa ya mwaka 2014 tulifanya vizuri lakini mwaka huu tuikatae asilimia hiyo tufikie asilimia 100” alisema Dkt. Nchimbi.
Dkt.Nchimbi alisema bila ya kuwa na afya hakuna litakaloweza kufanyika hasa katika kipindi hiki ambacho taifa letu linaingia kwenye uchumi wa kati wa viwanda.
Alisema magonjwa hayo ya surua rubella na polio ambayo yanaenezwa kwa hewa hayabagui jinsia ya mtu, taaluma yake, utaifa wake, uongozi wake na fedha zake hivyo ni muhimu kila mmoja wetu kuzingatia kampeni hiyo ili kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini.
Dkt. Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa dini ambao ni wajumbe wa kamati hiyo kuiombea kampeni hiyo na kwenda kuwahimiza waumini wao kuwapeleka watoto wao kwenye chanjo hiyo itakayofanyika kitaifa kuanzia Oktobata 15/19 2019 kwa kuwapeleka watoto wao wenye umri wa miaka mitano kushuka chini.
Aliongeza kuwa kampeni ya chanjo hiyo haina itikadi ya chama chochote ni kampeni ya watu wote walio Tanzania na Mkoa wa Singida.
Mtaalamu wa Jinsia na Utetezi kutoka Shirika la World Vission Tanzania, Tumaini Fred aliomba wakati wa kampeni hiyo watumishi wapewe muda wa nusu saa kwa ajili ya kuwapeleka watoto wao kupata chanjo kwani uzoefu umeonesha watoto wao hawakupatiwa chanjo kutokana na wazazi wao kukosa muda wa kuwapeleka.
Katika kampeni ya mwaka huu Mkoa wa Singida umelenga kuwafikia watoto 225,586 kwa chanjo ya Surua-Rubella na pia watoto 119,198 watapatiwa chanjo dhidi ya polio kwa njia ya sindano.