Sehemu ya washiriki wa Maadhimosho ya Siku ya Amani Duniani wakifuatilia
matukio.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene akiwa na viongozi wengine kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Jukwaa la Mabadiliko ya Tabianchi Rebeca Muna, Mkurugenzi wa Mashtaka
Biswalo Mganga, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN)-Tanzania Amon
Manyama na Clara Makanya kutoka Shirika la Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene
akivishwa skafu na skauti alipowasili katika tukio hilo.
Picha ya pamoja ikiwahusisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (walioka katikati)
mara baada ya kuhutubia Maadhimisho hayo.
**********************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene amesema mabadiliko ya tabianchi nchi huathiri moja kwa moja
shughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii hivyo huatarisha amani.
Akizungumza kwenye kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani
yaliyofanyika Jijini Dodoma Septemba 21 Mhe. Simbachawene ambaye alikuwa
mgeni rasmi alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi huchangiwa na
shughuli za kibinadamu.
Alisema kuwa shughuli hizo husababisha kuongezeka kwa halijoto, kupungua
kwa kiwango cha mvua, kukauka kwa vyanzo vya maji na kuongezeka kwa
magonjwa ya binadamu, wanyama na mimea.
"Kwa kiasi kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi huchangiwa na shughuli za
kibinadamu zikiwemo uchafuzi wa hali ya hewa, uchomaji misitu, ukataji miti bila
kuotesha na shughuli za kilimo na ufugaji zisizozingatia uhifadhi wa mazingira
ambazo huchangia kuongezeka kwa hali ya joto," alisema Waziri huyo.
Aliongeza kuwa pamoja na athari za mabadiliko haya kuzikumba nchi zote
duniani pia huzikumbwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na hi ni kutokana
na ukeli kuwa ukuaji wa uchumi wetu hutegemea zaidi shughuli za kiuchumi.
Kutokana na hali hiyo Waziri huyo alibainisha kuwa ili kukabiliana changamoto
hizo kama nchi tunahitaji kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuhimili na
kujiepusha na majanga yanayosababishwa nayo.
Alitahdharisha kuwa majanga yanayotokana na hali hiyo husababisha hasara za
kiuchumi na kijamii zinazochangia kuongezeka kwa umaskini na hata migogoro
ya kijamii.
“Chanzo cha kupotea kwa amani kwa baadhi ya maeneo ni chanzo chake ni
mabadiliko ya tabianchi na hali ikibadili watu wakakosa mahitaji kama maji
hawawezi kukubali kufa lazima watatumia nguvu yoyote kuyapata kwa
kugombana.
“Hali ya hewa ikibadilika kusababisha kukosekana kwa maji watu watapambana
na kutafuta yake kidogo yaliyopo na katika kuyatafuta lazima watagombana hivyo kusababisha vurugu hivyo amani ina uhusiano mkubwa na mabadiliko ya
tabianchi”alisema.
Mhe. Simbachawene alidokeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa mazingira
hivyo imeendelea kufanya jitihada kubwa za kutunza na kusimamia mazingira
kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ukuta wa kingo za bahari.
Kwa upande mwingine Waziri Simbachawene alihimiza jumuiya za kimataifa
kuweka mkazo katika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi kwa
kuzingatia kuwa uchumi wetu hutegemea shughuli zitokanazo na mazingira.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN)-Tanzania Amon
Manyama alipongeza Serikali kwa jiihada zake za kulinda amani hususana katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kuwa ni jambo jema kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na
changamoto hiyo na kuwa amani ni msingi wa kuanzishwa kwa UN hivyo
tuhakikishe jitihada hizi zinadumu.