Home Mchanganyiko TAMA KAGERA YA TAMBULISHA  MRADI MPYA WA PETS

TAMA KAGERA YA TAMBULISHA  MRADI MPYA WA PETS

0

Na Silvia Mchuruza,Kagera.
 Shirika lisilo la kiserikali  Tanzania Agricultural Mordenization Association (TAMA) mkoani kagera limetamburisha mradi mpya wa PETS unaoshughurika na ufuatiliaji wa rasilimali zinazowafikia wananchi kwa njia ya kilimo.
Akizungumza na washiriki na wadau wa kilimo DAS Kadole Kilugara kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba amewataka viongozi wote Madiwani na maafisa kilimo wa kata 6 sita zinazopitiwa na mradi huo kuonesha ushirikiano wa kutosha.
“Inabidi kuhakikisha viongozi wote mnatoa ushirikiano wa kutosha pia mradi huu hautafanikiwa kama madiwani na maafisa ugani amtatoa ushirikiano mzuri” amesema DAS  Kadole.
Pia ameongeze  kuwa licha ya shirika hilo la TAMA ambalo limeanzisha mradi  PETS inawabidi kuwasilisha taarifa zote za mradi kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya  ya Bukoba.
Kwa upande wake Afisa kilimo umwagiliaji na ushirika Bw.Deogratus Mshauli kwa niaba ya mkurugenzi  wa halmashauli ya wilaya ya Bukoba ameeleza kuwa wananchi watashirikishwa ili kuweza kujua miradi inayotekelezwa katika maeneo hayo ili  kutimiza dhana ya utawala bora.
Awali  mwezeshaji wa mradi huo Ndg.Godfrey Mwegesela amesema kuwa kupitia mradi huo utajihusisha na ufuatiliaji wa huduma bora na maendeleo kwa ujumla.
“Kupitia mradi huu tutaboresha upatikanaji wa huduma za kilimo na kuongeza upatikanaji wa mazao na chakula bora lakini pia kupitia mradi huu tunawaweka karibu wakulima katika maeneo yao kwa kushirikiana na maafisa ugani wao” amesema Ndg.Godfrey.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa asilimia 70% ya wananchi nchini wanategemea kilimo na ndio maana wamechagua kata sita za halmashauli ya bukoba ambazo ni  Kemondo, Katerero, Nyakato, Maruku, Karabagaine,  na Kishanje ambapo mradi huo utaanza mwezi wa 9 mwaka huu mpaka mwezi wa 3 mwaka 2020.
Baadhi ya Madiwani kutoka katika kata 6  pamoja na maafisa ugani wameahidi kutoa ushirikiano  kwa shirika hilo la TAMA kupitia mradi wao wa PETS unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni  kwa lengo la kukuza sekta ya kilimo kupitia kwa wakulima ambao mradi upo katika maeneo yao.