Home Mchanganyiko TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

0

KUPATIKANA NA NISHATI YA MAFUTA BILA KIBALI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na Operesheni, Misako na Doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya katika kuzuia na kupambana na uhalifu na kudhibiti uuzaji na usambazaji wa nishati ya mafuta bila kibali.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa kumi na sita [16] kwa tuhuma za kupatikana na kufanya biashara ya nishati ya mafuta aina ya Diesel na Petrol bila kibali.

Katika misako iliyofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba, 2019 hadi 19 Septemba, 2019 katika maeneo ya Maghorofani, Uyole, Itezi Jijini Mbeya, Chimala, Igawa na Igurusi Wilayani Mbarali na maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyela na Chunya jumla ya watuhumiwa 16 wamekamatwa na jumla ya lita 5,940 za Diesel na lita 20 za Petrol zimekamatwa.

Aidha katika misako hiyo watuhumiwa wamekutwa na madumu 79 na mapipa 06 yenye ujazo tofauti tofauti yanayotumika kuhifadhia mafuta hayo pamoja na mipira ya kuhamishia mafuta.

Watuhumiwa waliokamatwa ni:-

 1. MAJALIWA EDWARD [30] Mkazi wa Mwambene
 2. EDSON KALINGA @ MANGI [32] Mkazi wa Iganzo
 3. HAMIS ANYIMIKE [32] Mkazi wa Mafiati
 4. ISSAH MWAMBELO [33] Fundi Magari na Mkazi wa Sae
 5. KAMBELA HAMAD MWIPOPO [30] Mkazi wa Makunguru
 6. LUGANO MWASALEMBA [18] Mkazi wa Kibonde Nyasi.
 7. DAUD MWASALEMBA [40] Mkazi wa Itezi
 8. SIKUDHANI ANTHONY [35] Mkazi wa Kijiji cha Isyonje
 9. HASHIM DAVID JOSEPH [20] Mkazi wa Mchangani
 10. JUSTINE ADAM [21] Mkazi wa Isyonje
 11. GEORGE MWAKALOBO @ MWADADA [40] Mkazi wa Ipinda
 12. MAJUTO SIMONI [37] Mkazi wa Kapwili
 13. LWITIKO MWAIPOPO [38] Mkazi wa Ipinda
 14. JAKOBO MWAKILEMA [47] Mkazi wa Ipinda
 15. ANGALWISYE ASUBISHI [35] Mkazi wa Chimala 
 16. MWAGAMBO USWEGE [40] Mkazi wa Igurusi

Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

KUINGIZA BIDHAA NCHINI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.


Mnamo tarehe 16/09/2019 majira ya saa 03:30 usiku huko maeneo ya Imezu, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Askari Polisi waliikamata gari namba T. 667 ADM aina ya Mark II rangi nyeupe na baada ya kuikagua ndani yake ilikuwa na vipodozi vya aina mbalimbali ambavyo ni:-

 1. Carolite dozen 24 na pic 52, 
 2. Betasol pic 90,
 3. Diproson pic 20,
 4. Epiderm pic 30,
 5. White Max boksi 02,
 6. Diana Lotion boksi 02,
 7. Cocoderm pic 12,
 8. Teint Claire pic 06,
 9. Esapharma Dozen 48 na pic 10,
 10. Lemovet Cream Dozen 46 na pic 10,
 11. Clairmen pic 72,
 12. Extra Clair pic 77,
 13. Citrolite Dozen 12 pic 18,
 14. Calorite Dozen 24 na pic 52,
 15. Top Lemon pic 24,
 16. Carats pic 32,
 17. Miki Clair Dozen 4,
 18. Mount Clair Dozen 1,
 19. Bronz Dozen 2,
 20. Clinic Cleare dozen 3,
 21. Bio Claire dozen 1,
 22. Dodo Dozen 1 na pic 2
 23. Carotone pic 6 na
 24. Actif Plup pic 1 ambavyo ni vipodozi vilivyopigwa marufuku kuingia nchini.

Mbinu iliyotumika ni dereva asiyefahamika kupita kwa spidi maeneo ya maghorofani kitendo kilichopelekea kutiliwa shaka gari hilo na askari Polisi kisha kuifuatilia gari hiyo na kuikamata ikiwa na vipodozi hivyo. Msako mkali wa kumtafuta dereva wa gari hilo na mmiliki wake unaendelea. 

KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.

Mnamo tarehe 16/09/2019 majira ya saa 03:30 usiku huko maeneo ya Imezu, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, askari Polisi waliikamata gari namba T. 667 ADM aina ya Mark II rangi nyeupe na baada ya kupekua ndani yake kulikuwa na vitenge jozi 106 na mabelo 03 ya vitenge ambayo hayajafunguliwa vikiwa vimeingizwa nchini bila kibali. 

Mbinu iliyotumika ni dereva asiyefahamika kupita kwa spidi maeneo ya maghorofani kitendo kilichopelekea kutiliwa shaka na askari Polisi na kuanza kuifuatilia gari hiyo na kuikamata ikiwa imebeba vitenge hivyo. Mtuhumiwa mmoja aitwaye HOBOKELA MWAKYUSI JENGELA [49] Mfanyabiashara na Mkazi wa Sae anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na bidhaa hizo. Msako wa kumtafuta na kumtia mbaroni dereva na mmiliki wa gari hiyo unaendelea.