SERIKALI imetangaza ajira mpya kwa watumishi 477 kwa kada ya Afya ambao watawasaidia kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Tanga Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo alisema kwamba Tamisemi imepata kibali cha ajira ya watumishi hao Julai 12 mwaka huu na utekelezaji wake ulianza Julai 22 mwaka huu kwa kutangaza nafasi hizo.
Alisema kwamba walitangaza nafasi hizo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa maombi ya kazi kwa ajili ya waombaji wenye sifa kuomba nafasi hizo ambapo maeneo 14 walikuwa wakihitaji watumishi waweze kuwasaidia kwenye mamlaka za serikali za mitaa.
Alisema kwamba eneo la kwanza ni kupata madaktari daraja la pili ambao walihitajika 44,tabibu daraja la pili 100 ,tabibu msaidizi 19,Afisa Muuguzi daraja la pili 5,afisa muunguzi msaidizi daraja la pili 33,muunguzi daraja la pili 119,tenkolojia daraja la pili upande wa maabara 3.
Aidha alisema kwamba maeneo mengine ni teknolojia msaidizi wa maabara 4,teknolijia daraja la pili kuhusu dawa wanne, teknolojia daraja la pili upande wa mionzi 44,mtoa tiba kwa vitendo daraja la pili 1,Afisa afya mazingira daraja la pili 8,Afisa Afya Mazingira msaidi daraja la pili 29 .
Waziri Jafo alisema kwamba nafasi nyengine ni wahuduma wa afya 64 huku akieleza kwamba zoezi la uchambuzi huo lilianza Agosti 12 mwaka huu hadi 28.8,2019 ambapo jumla ya waombaji wote walikuwa 20237.
Alieleza kwamba kati yao waliomba wenye sifa ni 2644 na waombaji 17593 hawakuwa na sifa za kuajiriwa kwa mujibu wa tangazo la ajira kutokana na sababu mbalimbali kama ikiwemo uchambuzi wa sifa ambao ulizingatia mambo sita .
Alisema jambo la kwanza ni uwepo wa nakala ya kidati cha nne au sita, pili uwepo wa nakala za cheti cha taaluma na tatu uwepo wa nakala ya cheti cha kuzaliwa, uwepo wa nakala ya cheti cha usajili kamili au leseni ya kufan ya kazi inayotolewa na mabaraza ya kitaalamu.
Aidha alisema pia kwamba lazima uwepo wa nakala ya vyeti v ya kidato cha nne au sita na uwepo wa nakala ya cheti cha nacte kwa waombaji wote wa ngazi za cheti na diploma kwa waombaji wote ya koazi husika kwa waliomaliza septemba 2015 na kuendelea.
Alisisitiza kwamba hivyo vilikuwa miongoni mwa vigezo kwa waombaji hao 17593 wengine waliowasilisha taarifa zao zikiwa na mapungufu ya hapa na pale wakati wanafanya uchambuzi kwenye baadhi ya changamoto kulikuwa na waombaji wengi.
Alisema pia uwepo wa waombaji wachache kwa kada ya mionzi wakati waliotangaza walikuwa wakihitaji watu wa mionzi 44 lakini walioomba walikuwa 46 lakini kati ya hao waombaji 25 ndio walikuwa wana sifaa na 19 waombaji walikuwa wamepungukiwa na sifa pia uwepo idadi kubwa ya waombaji wasiokidhi vigezo.
“Niwapongeze waombaji wote waliopata nafasi na nisistiza maekelezo yafuatayo kuripoti kwenye vituo vya kazi kwa muda wa siku kumi na nne kuanza leo hii na wale ambao watashindwa kufanya hivyo nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine haraka sana”Alisisitiza.
Hata hivyo aliwakumbusha kuhakikisha wakati wa kuripiti wanakwenda na vyeti halisi vya kidato cha nne,sita ,chuo kikuu,nacte na vyeti halisi vya usajili wa baraza la kitaalumu ambao watapaswa kuwasilisha kwa mwajiri kabla ya kupata barua ya ajira.
“Lakini pia niseme kwamba kuripoti na transcript pekee bila kuwa na cheti halisi hatopokelewa hivyo ni muhimu waliotangazwa waende na vyeti vyao halisi na watakaoshindwa kuwasilisha vyeti watakuwa wamekosa sifa”Alisema
Waziri huyo alisema kwamba watawapeleka kwenye maeneo yenye changamoto ya watumishi ambao wameomba na kutokupata fursa wasisite kuomba tena huku akiwataka wakurugenzi kuwapokea na kuhakiki vyeti vyao ikiwemo kuwapatia mafunzo .