Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na kiongozi wa madaktari wa shirika la Sharjah Charity Group kutoka nchi za Falme za Kiarabu Ahmed Mohammed Alkamali alipofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari hao kwa kushirikiana na madaktari wa JKCI leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda
Kutoka kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakimsikiliza Daktari kutoka Shirika la Sharjah Charity Group wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akifurahi pamoja na mmoja wa watoto wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati), Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi (kulia) pamoja na Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi wakimpatia zawadi mtoto mwenye magonjwa ya moyo anayepata matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa zawadi daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Shirika la Sharjah Charity Group kuwapongeza kwa jitihada wanazozifanya kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa ngao Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi kuthamini mchango unaotolewa na shirika hilo kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa ngao Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyotolewa na taasisi ya Islamic Foundation Tanzania kumpongeza kwa jitihada anazozifanya katika kuboresha huduma za matibabu ya moyo katika taasisi hiyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali na watoto wenye magonjwa ya moyo wanaopata matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa waziri ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi
Picha na: Genofeva Matemu – JKCI